Pages


Photobucket

Saturday, January 18, 2014

KAMPENI ZA UDIWANI MBUNGE WA CHADEMA AJIKUTA AKIJIHUTUBIA MWENYEWE NA WASHIKAJI ZAKE ALIOENDA NAO ONA NOMA HII LIVE!!




Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni za chadema kata ya Nduli, Iringa, leo

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema


Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano huo












Na Francis Godwin Blog
IKIWA ni siku mbili toka katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Hassan Mtenga kumwagiza mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kufuatilia kero mbili za wananchi ikiwemo ya wagonjwa kukosa dawa katika Hospital ya mkoa na kujua fedha za ruzuku ya jimbo la Iringa mjini ziko wapi na zinafanya nini, mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna kiasi cha Tsh milioni 30 nyingine za mfuko wa jimbo.

Huku mbunge Msigwa akiwaomba radhi wananchi wachache waliofika katika mkutano huo kwa kudai kuwa haukutangazwa vya kutosha .

Hatua ya katibu huyo kuagiza kufuatilia fedha hizo ni baada ya jimbo hilo kukabiliwa na changamoto mbali mbali na fedha hizo zinazotolewa na Rais zimelenga kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini Manispaa ya Iringa fedha zinakaa bila kazi.

Akizungumza katika mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli leo ,Msigwa alisema kiasi hicho cha Tsh 30m zipo hadi sasa.

“Naomba kuwahakikishieni nitaendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kusaidia kero za maji hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe Ayub Mwenda nitafanya nae kazi”

Pia Mbunge Msigwa amesema kuwa katibu wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake ila yeye saizi yake ni akina waziri mkuu Mizengo Pinda,waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani Wiliam Lukuvi na katibu mkuu wa CCM Bw Kinana na sio yeye .

“Nataka kuwahakikishia kuwa huyu mimi si saizi yangu saizi yake ni akina Frank Nyalusi diwani wa Mvinjeni (Chadema) na katibu mwenzake wa Chadema Iringa mjini Suazana Mgonakulima.

Wao wanasema amekuja kwa ajili ya kunishughulikia mimi ila nasema njia aliyojia atatitoka na njia hiyo hiyo kama walikuwepo akina Charles Charles na wametoka zaidi ya makatibu 7 iwe yeye .

Hata hivyo katika mkutano huo ambao idadi ya watu ilionekana ni ndogo zaidi ukilinganisha na hali halisi ya nguvu ya Chadema iliyokuwepo jimbo la Iringa mjini ,bado mbunge huyo alitumia mkutano huo kuwaomba radhi wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi kwa madai haukutangazwa vya kutosha.

Kampeni za uchaguzi mdogo wa kata hiyo ya Nduli zimeanza rasmi leo kwa Chadema kufungua pazia hilo huku wao CCM wanataraji kuzindua kampeni hizo katika eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu

Uchaguzi huo mdogo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Idd Rashid Chonanga aliyefariki duni kwa ugonjwa mapema mwaka jana.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa Chadema katika kata hiyo ya Nduli Ayub Mwenda ambae alipata kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Nduli kabla ya CCM kumsimamisha nafasi hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za maendeleo ,alisema kuwa yeye ana risiti za fedha zote ambazo alikuwa akikusanya na kuwa kusimamishwa kwake nafasi ya uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Lusiana Mbosa na kuwaomba wananchi kumkubali sasa ili awe diwani wa kata hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Iringa wanadai kuwa kipimo cha kukubalika ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo hilo kwa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi za serikali za mitaa ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli

No comments:

Post a Comment