Mkurugenzi mkuu wa shirika la BBC, George Entwistle, amejiuzulu.
Amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.
Taarifa
hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali
ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya
kudhalilisha watoto.
Tayari
shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu
mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha
watoto.
Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.
Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".
Akisimama
kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa
moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".
"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"
"Kama
Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George
amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu
ambayo umezua malalamiko mengi".
No comments:
Post a Comment