By Majid Ahmed, Mogadishu
Wakazi wa Mogadishu wanafanya jukumu kubwa katika usafishaji wa mabaki
ya al-Shabaab katika mji mkuu, maofisa wa usalama wa Somalia wamesema.
Washukiwa wa Al-Shabaab wakipanda katika
gari ndogo ya wazi ya polisi tarehe 10 Oktoba, mwaka 2012 katika kituo
cha polisi huko Mogadishu ya kusini. [Abdurashid Abdulle Abikar/AFP]
Fununu kutoka kwa wakazi katika eneo la Yaqshid huko Mogadishu ya
kaskazini Jumamosi (tarehe 24 Novemba) ilisababisha katika kukamatwa kwa
washukiwa 21 wa al-Shabaab na ugunduzi wa maficho ya silaha, kwa mujibu
wa maofisa usalama.
Siku mbili kabla, vikosi vya usalama vilifanya operesheni kutokana na
fununu kutoka kwa mmiliki wa shamba huko Yaqshid ambayo matokeo yake
ilikuwa mauaji ya kamanda wa al-Shabaab Abdinur Gardhub . Operesheni ya
tarehe 22 mwezi Novemba pia ilisababisha kukamatwa kwa wanamgambo
wengine 16 ambao walifanya shughuli nje ya kikundi kidogo cha watu
katika maeneo ya Yaqshid, Suqa Holaha na Gubta, kwa mujibu wa kamanda wa
Idara ya Usalama wa Taifa huko Benadir Koloneli Khalif Ahmed Ereg.
Ereg alisema maficho ya al-Shabaab huko Yaqshid yaligundulika kutokana na taarifa zilizotolewa na wakazi wa eneo hilo.
"Vikosi vya usalama viliwatia kizuizini wanachama 37 wa kikundi cha
wapinga amani wa al- Shabaab, wakati wa mfululizo wa mashambulizi ya
usiku yaliyofanywa kitongoji cha kaskazini ya Mogadishu," Ereg aliiambia
Sabahi. "Mashambulizi haya yalilenga katika usafishaji wa mabaki ya
al-Shabaab katika eneo hilo."
"Operesheni hizi zilisababisha kunyang'anywa kwa maficho ya aina tofauti
za silaha ikiwa ni pamoja na silaha za vita, bunduki AK-47, silaha,
milipuko na maguruneti ya kurusha kwa mkono," alisema.
Ereg alisifu ushirikiano wa wakazi pamoja na vikosi vya usalama.
"Tunathamini ushirikiano wa raia na vikosi vya usalama wakati wa
operesheni za hivi karibuni ambazo zilisababisha kukamatwa kwa wanachama
wa al-Shabaab na ugunduzi wa maficho ya silaha zilizokuwa zinamilikiwa
na wanamgambo hao," alisema.
Serikali ya Somalia ilitangaza mwishoni mwa mwezi Aprili kwamba ingetoa
hadi dola 500 kwa wananchi watakaojitokeza na taarifa zitakazosaidia
kukamatwa au kuuawa kwa wanachama wa al-Shabaab.
Wananchi wapo tayari kusaidia jitihada za usalama
Mzee wa Mogadishu Suleiman Abdullahi alisema kwamba kupigana na
wanamgambo ambao wanavuruga usalama wa Somalia ni wajibu wa kidini na
kitaifa.
"Vikosi vya usalama wa taifa, polisi na jeshi wote wanafanya kazi
inayotakiwa ya kusafisha mji na maeneo yanayozunguka ya wanamgambo,"
aliiambia Sabahi. "Tunawapongeza katika operesheni hii yenye mafanikio
ambayo italeta utulivu zaidi huko Mogadishu, na tupo tayari kutoa msaada
kwa vikosi vya usalama."
"Magaidi wanaishi miongoni mwetu na kwa bahati mbaya kuna wale wanaowapa
kimbilio salama," alisema Abdullahi. "Kama tunataka kuishi kwa utulivu,
amani na usalama, tunapaswa kushirikiana na vikosi vya usalama ili
kulinda usalama wetu na pia tunapaswa kutowapa makazi magaidi kwa sababu
inamaanisha tunajisaliti sisi wenyewe, taifa letu na nchi yetu kwa
ujumla."
Osman Mohamed, kanali mstaafu wa polisi Somalia, alisisitiza umuhimu wa
kujenga ujasiri na kushirikiana kati ya wananchi na vikosi vya usalama.
Alisema hii ni sababu ya msingi katika mafanikio ya jitihada za polisi
na vikosi vya usalama kuendeleza utulivu huko Mogadishu na maeneo
mengine yaliyokombolewa hivi karibuni.
"Kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi na wafanyakazi wa usalama
kunachangia kuelekea katika uimarishaji wa imani ya umma kwa vikosi vya
usalama na kuleta kujisikia kuridhika kwa jitihada zao," Mohamed
aliiambia Sabahi.
Alisema vikwazo ambavyo vilikuwepo zamani kati ya wananchi na vikosi vya
usalama sasa havipo tena. "Vikosi vya usalama vimefanikiwa kwa kiwango
fulani kuiteka mioyo na mawazo ya wananchi kwani watu hawaogopi tena
vikosi vya usalama na sasa mawasiliano kati ya pande zote yako imara,"
alisema.
Kuendeleza usalama ni wajibu wa pamoja
Kaimu Gavana wa Masuala ya Usalama wa Benadir Warsame Mohamed Hassan
alisema ushirikiano kati ya vikosi vya usalama na wananchi katika
kutafuta watu ambao wanavuruga usalama wa umma ni muhimu.
"Shukrani kwa ushirikiano kati ya wananchi na vikosi vya usalama, hali
ya usalama huko Mogadishu imeboreshwa kwani viwango vya mauaji na
vitendo vya kuvuruga usalama vimepungua kwa wiki chache zilizopita,"
Hassan aliiambia Sabahi.
Alitoa wito kwa jamii kwa ujumla kuwajibika katika jitihada
zinazoendelea zinazokusudia kudhibiti usalama na kuendeleza utulivu huko
Mogadishu.
"Majeshi ya usalama hayawezi kufanya kazi yake ya kuendeleza hali ya
usalama na kusafisha Mogadishu dhidi ya al-Shabaab bila ushiriki wa
jamii," alisema. "Kuimarisha usalama ni wajibu wa pamoja na kila mmoja
anapaswa kuwajibika katika hili."
Hassan alisema operesheni za usalama zingeendelea huko Mogadishu hadi
mji uwe huru dhidi ya al-Qaeda wanaoshirikiana na wanamgambo wa
al-Shabaab.
Chanzo sabahionline.com
Chanzo sabahionline.com
No comments:
Post a Comment