BAADHI ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wafafanua aina za rushwa
zinazotokea katika tasnia ya muziki ambazo zinasababisha kudidimiza
muziki pamoja na vipaji vya wasanii.
Rushwa hizo ambazo zinatolewa na baadhi ya wasanii kwa baadhi ya vyombo
vya habari kwa ajili ya kupiga muziki wa msanii hata kama hauna
sifa,imezidi kuchukua sura mpya kwa kuhusisha baadhi ya mashabiki kwa
ajili ya kuomba nyimbo katika radio.
Akifafanua aina ya rushwa hizo jijini Dar es Salaam Hugoline Martin 'Dj
Choka' ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Bongo Star alisema, kuna aina
mbili za rushwa ambapo moja ilikuwa imezoeleka kwa wasanii kutoa hela
kwa baadhi ya watangazaji wa redio ili kuwezesha nyimbo zao kupigwa
kwenye vipindi ambapo rushwa hii imezoeleka kwa baadhi ya wasanii walio
wengi nchini.
Kutokana na hali hiyo alisema muziki wa bongo fleva unakuwa kwa
kusikilizwa kwa wingi kwenye baadhi ya vyombo vya habari huku ukiwa
unakosa sifa ya ubunifu hali inayochangia kufanana kwa baadhi ya nyimbo
kuanzia melody hadi mahudhuhi ya nyimbo.
Alisema kuwa rushwa ya aina ya pili ni ile ya mashabiki ambao wanapewa
hela na baadhi ya wasanii kwa ajili ya kuomba nyimbo redioni hali ambayo
inaonyesha msanii fulani nyimbo yake kuombwa mara kwa mara hata kama
haina sifa na imekosa ubunifu.
"Kuna rushwa nyingi sana kwenye muziki sasa kuna hii mpya ya baadhi ya
wasanii kutoa hela kwa mashabiki wao ili kuomba nyimbo kwenye redio
kwahiyo utaona nyimbo inaombwa sana hata kama haina sifa hii
inasababisha kuushusha muziki wetu " alisema Choka
Akielezea kwa upande wake jinsi anavyofanya kazi na wasanii hao wa
muziki wa bongo fleva alisema, ameweka vigezo kwa wasanii hivyo haweki
nyimbo ambayo haina vigezo kwenye mtandao wake.
"Nimeshakataa kupigiwa simu na wasanii kuniomba niweke nyimbo yake
kwenye mtandao wangu na mimi sipokei hela teyari wanafahamu hilo hivyo
muziki ninaouweka kwenye blog ni ule wenye sifa na vigezo tu na siyo kwa
ajili ya hela " alisema Choka
Kwa upande wake msanii wa bongo fleva kutoka kundi la TMK wanaume Amani
Temba anayejulikana kwa jina la 'Mheshimiwa Temba' amesema kunatofauti
kwa upande wa muziki kwa kipindi hiki na kipindi cha zamani ambapo hapo
mwanzo muziki ulikuwa unasikika kwa nguvu ya prodjuza pamoja na msanii
mwenyewe.
Alisema rushwa imejaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari ambapo msanii
nyimbo yake haipigwi mpaka atoe hela sababu inayosababisha kuwa na
nyimbo nyingi kusikika redioni huku zikikosa sifa ya kuwa nyimbo bora .
No comments:
Post a Comment