Viongozi wa nchi 11 za Afrika
wanakutana mjini Kampala, Uganda, kujaribu kutafuta suluhu katika vita
vya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Wapiganaji mashariki mwa Congo
walisonga mbele zaidi ndani ya ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na jeshi la
serikali siku ya Alkhamisi.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa awali
juma hili iliishutumu Rwanda kuwa inawasaidia wapiganaji hao, shutuma
ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.
Kiongozi wa kiraia wa kundi la wapiganaji wa M23 piya yuko kwenye mkutano wa Kampala.
Haijulikani mchango wake ni wa kiasi gani kwenye mkutano huo wa dharura wa viongozi wa kanda ya Maziwa Makuu.
Wapiganaji wanataka kuzungumza ana kwa ana na serikali ya Congo.
Lakini Rais Joseph Kabila anasema atazungumza tu na Rwanda.
Huku nyuma wapiganaji wanaendelea kusonga mbele wakielekea kusini na kaskazini kutoka shina lao mjini Goma.
Umoja wa Mataifa unasema kikosi chake kilioko
huko kitajaribu kuwazuwia wapiganaji wasisonge mbele, lakini umesema
askari wake wa kuweka amani hawawezi kubeba jukumu la jeshi la serikali
ya Congo.
Na bbc swahili
No comments:
Post a Comment