Bi Arafa Issa Namaji(Pichani) mwenye
umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani
Lindi anaomba msaada wa haraka utakaomuwezesha kupata matibabu ya
uvimbe ulio katika paji la uso uliotokana na maumivu makali ya kichwa
baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Ndanda na kuelekezwa kufika
katika hospital ya Taifa ya Muhimbili(MNH) Kwa uchunguzi zaidi na matibabu.
Tatizo lilianza tangu mwezi february
2012, alianza kwa kuumwa na kichwakwa maumivu makali sana na kipele
kidogo kikatokea kwenye paji la uso, hivyo basi kadri kilipopungua
maumivu ndipo kipele kiliendelea kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na
sehemu ya pua baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya Majirani na
marafiki wa karibu walimshauri kwenda hospitali ya wilaya, alipofika
Daktari alimpa rufaa ya kwenda hopsitali ya Ndanda,hata hivyo Ndanda
pia wakampa rufaa kwenda hospitali ya Taifa muhimbili kwa uchunguzi
zaidi.kutokana na hali hali hiyo ngumu aliyonayo Kutokana na kuwa katika
hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ruangwa wameichangishana kupata kiasi cha nauli pamoja na hela kidogo ya
kujikimu kwa siku mbili, lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa
kwasababu atahitaji kuishi zaidi DSM Akiwa katika hospital ya Muhimbili
kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu yake Kwa alietayari kumsaidia
anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa
wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu0787176221 au 0756696048 Kutoa ni Moyo ili kumsaidia mama huyu
(Habari hii ni kwa Hisani ya Pwani Blog)
|
No comments:
Post a Comment