Mwendesha mashtaka mkuu nchini
Korea Kusini amejiuzulu, baada ya kuomba msamaha hadharani kushusiana na
kashfa kadhaa katika idara yake.
Han Sang-dae alisema matukio hayo,
yaliyowahusisha maafisa chini ya usimamizi wake, yaliwashangaza na
kuwavunja moyo watu wengi nchini humo.
Katika kisa kimoja, ofisa wa ngazi ya juu
ameshtakiwa kwa kupokea rushwa, huku mwingine ameshtakiwa kwa kupunguza
adhabu ya mshukiwa fulani na badala yake kuomuomba wawe wapenzi.
Chanzo ni BBC
No comments:
Post a Comment