Viongozi wa Afrika wamewasihi wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuacha mashambulio.
Mwisho wa mkutano wao mjini Kampala,
Uganda, viongozi hao wamewataka wapiganaji wa kundi la M23 waondoke
kutoka mji wa Goma waliouteka hivi karibuni.
Viongozi hao piya walimsihi Rais wa Congo, Joseph Kabila, kushughulikia malalamiko ya wapiganaji.
Viongozi wane walihudhuria mkutano huo - Rais Paul Kagame wa Rwanda hajakuwepo.
Walipendekeza kuweka kikosi cha pamoja katika
uwanja wa ndege wa Goma kitachokuwa na wanajeshi kutoka Tanzania, jeshi
la Congo na M23.
Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji wa M23 - shutuma inazokanusha.
Baada ya kuuteka mji wa Goma, wapiganaji wamesonga ndani zaidi kwenye ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na serikali.
Mashirika ya misaada yanaonya kuwa hali ya wakaazi inazidi kuwa
No comments:
Post a Comment