Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane
wa Chama cha Mapinduzi unaoendelea katika Ukumbi wa Kizota nje kidogo
ya Mji wa Dodoma juzi usiku walisahau tofauti zao juu ya wagombea
wanaowapigia debe kushinda nafasi wanazowania kufuatia hotuba ya
kusisimua iliyotolewa Mbunge wa Maswa Magharibi JOHN MAGALE SHIBUDA.
Licha ya SHIBUDA kuwa na kofia
ya Ubunge amefanikiwa kuhudhuria Mkutano huo wa CCM kufuatia mwaliko
alioupta kupitia wadhifa wake wa Ujumbe wa Mpango wa Utathmini Kiutawala
Bora kwa nchi za Afrika APRM ambao unasimamia pia masuala ya
demokrasia safi.
Akizungumza na Wajumbe zaidi ya
2000 na waalikwa takribani 4000, Shibuda amemtaka Rais JAKAYA KIKWETE
kusimamia elimu ya uraia ili kuondoa dhana ya chuki inayoendelea ndani
ya vyama vya siasa pale mwanasiasa mmoja anaposhirikiana na Watanzania
wenzake walio katika vyama pinzani.
SHIBUDA pia hakusita
kusikitishwa kwake na mdororo wa kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi
unaochangiwa na baadhi ya viongozi kutowafikia wananchama na badala yake
kutumia vyombo vya habari kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani
ambayo hayana msingi.Kuhusiana na viongozi kutowajibika katika
kutekeleza majukumu yao.
Mjumbe huyo pia anashindilia
hoja msumari kwa Rais KIKWETE na Serikali yake kuwa wasikifu pale
wapinzani wanapoibua changamoto za kimaendeleo na kuitumia fursa hiyo
kwenda kuzifanyia kazi ili kuwaondolea wananchi umaskini.
Kama anavyomalizia kwa kusema
‘Kaa la Moto Haliwekwi Mfukoni’ akatumia fursa hiyo pia kubainisha azma
yake ya kumtumia Rais KIKWETE na Rais wa Zanzibar DK ALLI MOHAMED SHEIN
katika kampeni zake za kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment