Makambi ya Ali Addeh na Holl-Holl huko Djibouti ni makaazi ya wakimbizi
wanaokadiriwa kufikia 25,000 pamoja na kuwa na changamoto kwa maofisa wa
serikali na mashirika ya kimataifa.
Awali ilijengwa kuwahifadhi watu 7,000,
kambi ya wakimbizi ya Ali Addeh huko Djibouti ambayo sasa inawahifadhi
wakimbizi 20,000, wengi wako katika mahema ya muda. [Harbi Abdillahi
Omar/Sabahi]
Hali ya wakimbizi huko Djibouti inabakia kuwa ya wasiwasi. Ukosefu wa
maji ya kunywa, utokeaji tena wa ukame, utapiamlo na uhaba wa chakula
vimefanya mchakato wa kuchanganyikana kwao kuwa mgumu, kwa mujibu wa
Aden Hassan wa Ofisi ya Taifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ajili ya
Msaada wa Wakimbizi na Watu wasio na Makaazi (ONARS), ambayo inasimamia
makambi hayo.
Kambi ya Ali Addeh, ambayo kwa sasa ni kambi kubwa ya wakimbizi huko
Djibouti, ilifungua milango yake mwaka 1991 baada ya serikali kuu ya
Somalia kuanguka. Ilijengwa kuwahifadhi wakimbizi 7,000, lakini kwa sasa
inawahifadhi kama 20,000.
Mwezi Disemba 2013, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) alikadiria kuwepo kwa wakimbizi zaidi ya 30,000 wanaoishi
Djibouti.
Katika jitihada za kupunguza msongamano, UNHCR na ONARS ilitaka serikali
kufungua tena kambi ya Holl-Holl, ambayo ilifungwa 2006. Ilifunguliwa
tena Juni 2012 na sasa inawahifadhi wakimbizi zaidi ya 1,000.
Ingawaje baadhi ya wakimbizi huko Djibouti wamesema wanataka kurudi
nyumbani mara nchi zao zikiwa na utulivu, wengi wangependelea
kuhamishiwa tena katika nchi ya tatu. Hadi mwaka huu, UNHCR iliwasaidia
kuhamishwa wakimbizi 225 huko Marekani, Uswidi, Kanada na nchi nyingine,
idadi iliyozidi 117 ya mwaka 2011.
Karibu asilimia 90 ya wakimbizi wa nchi wanatokea Somalia pamoja na wanaobakia wengi wao kutokea Eritrea na Ethiopia.
Wakimbizi wakabiliwa na maisha magumu kambini
Abdi Maalin, mkimbizi wa Somalia akiwa na miaka 30, amekuwa akiishi
katika kambi za Ali Addeh kwa miaka mitano. Aliiambia Sabahi kwamba
japokuwa al-Shabaab wamedhoofishwa, Somalia bado hakupo salama na
anamatumaini ya kufaidi kutokana na mpango wa uhamishaji.
"Leo sina uwezo wa kuendelea na masomo yangu ya chuo kikuu na siwezi
kufanya kazi nchini Djibouti kwa sababu sina kitambulisho chochote,"
Maalin alisema. Alisema watu wote wazima waliopo kambini wanakubwa na
ukosefu wa ajira na kukosa shughuli za kuwaingizia kipato.
Omar Idleh, mshauri katika Wizara ya mambo ya Ndani, alisema kuna
mahitaji ya kuongeza idadi ya vituo vya kupokelea wakimbizi na
kuwafundisha mtu mmojammoja kushughulikia vizuri wahamiaji katika
mateso.
"Nchi yetu inakabiliwa na wimbi kubwa la wakimbizi wanaoingia kutoka
mikoa tunayopakana nayo ya majirani zetu wa karibu katika majaribio ya
kufika rasi ya Uarabuni, ambako wanakuona kama El Dorado, hata kama
katika baadhi ya matukio inaweza kuwagharimu maisha," Idleh aliiambia
Sabahi.
"Kuwepo kwao katika nchi yetu ni mzigo mkubwa ambao unaleta ushiriki wao
katika uchafuzi, uharibifu na uchafu unaoharibu usalama wa mazingira ya
nchi nzima," alisema.
Amina Youssouf, mjane na mama wa watoto watatu mwenye umri wa miaka 42,
ambaye ameishi miaka 10 katika kambi ya Ali Addeh, alisema atahamia
Kanada mwaka 2013.
"Leo, sina mtu yeyote nchini Somalia," aliiambia Sabahi. "Wapendwa wangu
walifariki au kuhama nchini. Kwa hiyo kwa nini nihatarishe maisha yangu
na watoto wangu kwa kurejea tena?"
Alisema maisha katika kambi za wakimbizi yamekuwa ni mapambano zaidi ya
kukosa umeme na maji. "Watoto wangu hawakupata na elimu kwa sababu shule
ya msingi huko Holl-Holl imejengwa mwezi Septemba tu na iliyopo huko
Ali Addeh ina miaka minne tu," alisema.
Hata kama kungekuwa na shule, alisema, hakuwa na kitambulisho muhimu cha kuandikishia watoto wake shule.
"Ni mwezi Mei tu Shirika la Watoto la UN lilitambulisha vyeti vya
kuzaliwa kwa watoto wanaozaliwa, na uongozi huko Ali-Sabieh, ambao
unachukua kambi mbili za wakimbizi, lilianzisha vyeti vya kuzaliwa kwa
watoto wa wakimbizi wenye umri wa chini ya miezi minne, pamoja na sheria
za nyongeza kuwalinda wote wenye umri wa zaidi ya miezi minne,"
alisema.
Uhamiaji haramu pia ni hatari
Mahali ilipo Djibouti katika Bahari ya Shamu na ukaribu na Mashariki ya
Kati pia vinafanya uhamiaji haramu kuwa tatizo kuu kwa viongozi wa
Djibouti.
Ingawa sheria za Djibouti zinaruhusu wakimbizi kufanya kazi nchini,
kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na tatizo la chakula cha nchini
havisaidii mchanganyiko, Mkurugenzi Msaidizi wa ONARS Aden Hassan
aliiambia Sabahi. "Sehemu kubwa ya vijana na wakimbizi wa muda mrefu
ambao wanageuka kuwa wahamiaji haramu kwa sababu ya kutokuwa na mafunzo
na elimu na kwa sababu ya hali ngumu ya maisha."
Mwezi Agosti, UNHCR iliripoti kwamba uingiaji wa wakimbizi na wahamiaji
kutoka Pembe ya Afrika kwenda Yemen umevunja rekodi ya zaidi ya 63,800
katika miezi saba ya mwanzo ya 2012, ongezeko la asilimia 30 kutoka
rekodi ya awali mwaka 2011, wakati jumla ya wakimbizi 48,700 walivuka
mpaka.
Mkimbizi mmoja kati ya sita waliyovuka mpaka walikuwa Wasomali wakati
wengine walio wengi walikuwa Waethiopia. Idadi kubwa ya wakimbizi
walivuka kutoka mji wa bandari ya Djibouti wa Obock, UNHCR ilisema,
pamoja na ukumbusho kutoka mikoa ya Somaliland na Puntland ya Somalia.
No comments:
Post a Comment