Watu wawili wanadaiwa wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya kupigwa na watu wanadaiwa kuwa ni askari wa JWTZ.
Akizungumzia tukiohilo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMAN amesema
katika vurugu hizo mtu mmoja ndiye aliyeripotiwa amefariki dunia hadi
saa ambaye naye bado hajafahamika mara moja na kuongeza kuwa wengine
watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ifisi Mbeya.
hata
hivyo habari kutoka eneo la Tukio zinadai kuwa Novembeer 17 majira ya
saa tano za usiku ktk eneo la DDC mbalizi walinzi wakiwa kwenye doria
zao za maduka walimsimamisha askari mmoja wa JWTZ kisha kuanza kumpiga
hali iliyopelekea maumivu makali na kukimbilia kwenye kituo cha polisi
Mbalizi kwa ajili ya kutoa taarifa.
Badaa
ya kufika ktk kituo hicho alipewa huduma mara moja ambapo askari hao
waliondokana kwenda eneo la tukio na kuanza kufanya msako wa watu
waliohusika hata hivyo usiku hawakufankiwa kumkamata hata mmoja.
siku
inayofuata askari hao walifanikiwa kuwakamata walinzi watano na kuanza
uchunguzi mara moja ambapo siku hiyohiyo majira ya saa tano za usiku
askari wa JWTZ walivamia eneo hilo na kuanza kutembeza kipigo kwa
wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo kutokana na vurumai hizo watu wawili
waliumia vibaya na wengine kujeruhiwa.
aidha
watu hao walipelekwa ktk hospital ya Ifisi ambapo majira ya saa 5 siku hiyo
hiyo wawili kati ya hao waliokuwa wamepigwa walifariki dunia.
Hata
hivyo RPC DIWANI alisema kuwa uchunguzi unaendelea kwa ushirikiano wa
Polisi na JWTZ kuwapata waliohusika na tukio hilo la uvunjifu wa sheria.
Habari Chimbukoletu Blog.
No comments:
Post a Comment