KUTOKA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI URUSI.
Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za
msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya. Serikali kupitia bodi
ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi
,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi
mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.
Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa
Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu
, malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za
msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.
Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika
hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi
tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu
kama huna bima ya afya.
Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi
kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi
wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na
majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna
ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa
sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi
maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada
kwa wakati.
Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi
ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika
kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi
na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.
Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa
ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao
tupo hatarini huku ugenini.
Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia
na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa
ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3).
No comments:
Post a Comment