Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes mara
alipomtembelea Profesa Muhongo ofisini kwake. Balozi huyo
aliongozana na watendaji kutoka kampuni ya Koch Engineering & Construction
ya nchini Ujerumani ambao wanania ya kuwekeza katika miradi ya nishati ikiwamo
gesi asilia, umeme wa upepo, jua pamoja na kuwekeza katika viwanda vya
uzalishaji mbolea.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Balozi wa Ujerumani
nchini Tanzania Bw.
Klaus-Peter Brandes ramani ya bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mnazi
Bay Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Profesa Muhongo alimueleza
mheshimiwa Balozi kuwa Serikali ina mpango wa
kuzalisha umeme kwa njia ya gesi katika eneo la Somangafungu.
Picha na Afisa Habari Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment