Wafanyabiashara wakubwa wakionyesha bidhaa
zao katika soko la Wahen katika wilaya ya Gaan Libah ya Somaliland.
Utawala wa Somaliland inafanyia kazi kurahisisha taratibu za kuanza
biashara hapo kwa wajasiriamali. [Barkhad Dahir/Sabahi]
Mwongozo wa Uwekezaji wa Somaliland, umeanzishwa kwa ubia na Wizara ya
Biashara na Shirikisho la Biashara la Somaliland, Viwanda na Kilimo,
zitakuwa ni mahali pa kutatulia masuala ya uchumi, sheria, mamlaka ya
usajiri na taarifa za uwekezaji kwa wenyeji, waliotawanyika kwao na
wawekezaji wa kigeni.
"Tutaanzisha tovuti ya kukusanya taarifa kuhusu uwekezaji, fursa
zilizopo, mahali pa kuwekeza na taarifa zinazohusiana ili wawekezaji
wageni na waliotawanyika kwao na wananchi waweze kupata kwa urahisi
taarifa zitakazowasaidia kufanya uamuzi wakati wowote," alisema Mohamed
Saleban, mkurugenzi wa mipango na takwimu katika Wizara ya Biashara ya
Somaliland.
Tovuti pia itatoa taarifa kuhusu Somaliland, taratibu za kupata leseni,
viza zinazohitajika kwa wageni na taarifa zote zinazohusika, alisema.
Kufanyia kazi Mwongozo wa Uwekezaji wa Somaliland ulioanza mwezi Agosti
na utakamilika mwezi Januari mwaka 2013, kwa kutumia fedha kutoka
Shirika la Marekani kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa.
Aidha, serikali imeanzisha "eneo moja la biashara" kurahisisha
uwekezaji. Jitiahada, zinazofadhiliwa na Benki ya Dunia, zitaanzisha
ofisi moja ambayo inaleta pamoja mashirika kadhaa --ikiwa ni pamoja na
Wizara ya Biashara, Shirikisho la Biashara, Viwanda na Kilimo, Wizara ya
Fedha, na nyinginezo -- kurahisisha mchakato wa kupata leseni na kuwapa
wawekezaji taarifa zote wanazozihitaji katika sehemu moja.
Mradi huu, ambao utatekelezwa mwezi Januari, utasaidia wawekezaji kuokoa muda kwa kurahisisha mchakato wa usajiri, alisema.
"Ni fursa nzuri kuepusha vizuizi vyote," alisema Abdirahman Ismail, mkuu
wa idara ya mauzo katika Kampuni ya Telesom huko Hargeisa. "Kuwa na
eneo moja kwa ajili ya mfumo wa utoaji leseni kutapunguza usumbufu dhidi
ya muda unaopotea kujaribu kupata leseni kupitia mawakala mbalimbali."
"Tunakaribisha utekelezaji wake," aliiambia Sabahi. "Utawezesha mtu
yeyote anayependa kuanza kwa urahisi kufanya kazi huko Somaliland na
kufanya mchakato mrefu ambao mara haukushindika, ambao utaongeza uwezo
wa wawekezaji."
Kuondoa vikwazo katika kukua kwa uchumi
Mmiliki wa duka Asha Yusuf, ambaye anauza vifaa vya ujenzi huko
Hargeisa, alisema kurahisisha sheria na kufanya taarifa zipatikane zaidi
ni hatua katika mwelekeo sahihi, lakini kunahitajika kufanyika zaidi
ili kuhimiza wananchi kufungua biashara ndogondogo.
"Hitaji lao la kwanza ni kupata mikopo ambayo inafuata sheria ya kiislamu na sio kutoza faida," alisema.
Baadhi ya benki binafsi zimeanza kutoa mikopo midogo lakini zinahitaji
wakopaji kuwa na asilimia 30 ya kiwango cha mkopo kama malipo ya awali,
mahitaji ambayo wamiliki wa biashara hawawezi kukamilisha, alisema.
Serikali lazima iweke sera kusaidia biashara kupata fedha kwa ajili ya
gharama za kuanzia, alisema. Ni lazima pia itoe miongozo na msaada
mwingine unaohitajika ili wamiliki wapya wa biashara wasijisikie upweke
katika kufanya biashara kwenye uwekezaji mkubwa.
Saleban alisema Wizara ya Biashara inafanyia kazi programu ya kusaidia
utoaji fedha mdogo kwa ajili ya ubia wa umma na binafsi na itaendelea
kufanya kazi kuondoa vikwazo vinavyozuia kukua kwa uchumi.
"Lengo [la serikali] ni kuongeza uwekezaji, ambao baadaye utaongeza
ajira na kuboresha uchumi wa nchi," alisema. "Mara tutakapopata, kiwango
cha ubora wa maisha ya umma kinaweza kuongezeka."
Mabadiliko ya hivi karibuni yalikabiliwa na malalamiko kutoka kwa jamii
ya kibiashara na matokeo ya awali kutoka katika utafiti wa Ujasiri wa
Biashara wa mwaka 2012 huko Somaliland, ambayo yaliwasilishwa hadharani
tarehe 18 Disemba katika Mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa Biashara wa
Somaliland huko Hargeisa.
Utafiti ulitafuta maoni kutoka kwa wawekezaji na jumuiya ya
wafanyabiashara kuhusu mitazamo yao ya mazingira ya biashara Somaliland
na vikwazo katika uwekezaji, na ulifanyika Novemba huko Maroodi Jeeh,
Awdal, Sahil, Togdheer, Sool na Sanaag.
Utafiti ulipata majibu kutoka kwa wafanyabiashara 273 -- 236 kutoka
Somaliland na 37 waliotawanyika kwao -- ukijumuisha wanawake 72.
Utafiti ulionyesha kwamba asilimia 43 ya wahojiwa waliwekeza pungufu ya
Dola 10,000 kuanzisha biashara mpya huko Somaliland na asilimia 2.2 tu
wamewekeza zaidi ya dola milioni 1.
Uwekezaji ulitiliwa mkazo zaidi huko Maroodi Jeeh, Sahil na Togdheer,
ambako zaidi ya asilimia 20 ya biashara zilizotafitiwa ziliwekeza zaidi
ya Dola 100,000. Hata hivyo, huko Sool na Awdal, kiasi hicho kilishuka
hadi chini ya asilimia 8.
Kwa kuongezea, asilimia 58.5 ya wahojiwa walisema mchakato wa kusajili
biashara na kupata leseni ni mgumu, asilimia 43 walisema sheria za
kuanzisha biashara zingeweza kuwa na matokeo mazuri katika uamuzi wa
uwekezaji wa siku zijazo, wakati asilimia 21 walisema utakuwa na matokeo
hasi.
No comments:
Post a Comment