Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri
akikagua mradi wa maabara katika kituo cha afya cha Matai katika Wilaya
mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo amepiga marufuku miradi yote ya
serikali hususani inayohusisha mbao kupigwa rangi na badala yake ipakwe
vanish, hiyo ni kutokana na baadhi ya wakandarasi kutumia staili hiyo
kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe.
Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo
ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa na kukagua miradi
mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey
Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la mradi wa umwagiliji katika
kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri
aligoma kuweka jiwe la msingi katika mradi huu kutokana na mkandarasi
kujenga mradi huo chini ya kiwango kinyume na mchoro halisi wa mradi
huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Moshi Chang'a aweke jiwe hilo kwa niaba yake.
Kutoka kushoto ni Mama Mwanri mke
wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi
Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa katika picha ya pamoja pembezoni
mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika Hoteli ya Liemba Beach Resort
walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.
Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha
afya Matai mapema hii leo. Katika miradi miwili aliyotembelea Mhe.
Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo marekebisho aliyoagiza
yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa niaba yake.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Ndugu
Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa katika daraja la Mto Momba
linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu Mkoani Rukwa na wale wa
Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa kwa kamba limekuwa
halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba Serikali kuwajengea
daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao kirahisi.
Picha/Habari Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment