Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu
wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU),Dr. Salim Ahmed Salim
ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, mara baada ya Mh. Lowassa
kutoa maonai yake mbele ya tume hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba mpya,mara baada ya kutoa
maoni yake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Mjumbe wa Tume ya
Kukusanya Maoni ya Katiba mpya,Dk. Senkondo Mvungi mara baada ya kutoa
Maoni yake.
YAFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASAA:
Kwanza ningependa kukupongeza wewe
mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume nzima kwa imani kubwa ambayo
Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu hilo zito na muhimu kwa nchi
yetu.
Wananchi pia wamekuwa na imani
kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa tume hii. Kutokana na hilo
wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine hayahusiani na katiba, yaani siyo
ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa miongoni mwao, kwa hiyo naomba
radhi mapema, iwapo maoni yangu haya mengine , yataonekana si ya
kikatiba.
Katiba yetu ya sasa ni nzuri,
imetuongoza katika umoja na mshikamano wa kitaifa kwa muda wote
huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni vyema kuwepo na katiba
mpya ili kuendana na hali halisi.
Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.
1.ELIMU BURE
Moja ya haki za mtoto ni kupata
elimu. Ningependa suala la elimu bure ya sekondari liwemo kwenye katiba
yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya sekondari ni bure.Nchi yetu bado
ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni masikini.
Uwezo wao wa kipato ni
mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali inaweza kugharimia
elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya kujenga taifa lijalo
lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata elimu ya
sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.
Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa
watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo,
kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.
2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT
Katiba ya sasa haisemi wazi kuhusu
adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii
ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 inatamka kiujumla tu
kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI WAKE KULINDWA.
Lakini , haki hiyo inanyang'anywa
na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16(penal
code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya kifo(death penalty or capital
punishment) kwa kosa la mauaji ya kukusudia.
Adhabu hiyo hiyo pia utolewa kwa
kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni kwamba kuwe na ibara
katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA NA ADHABU YA KIFO
HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.
3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI
Katika sehemu nyingi hapa nchini
mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni kiasi gani cha fedha
ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika kampeni.Iainishe ni matumizi
gani ya lazima ambayo mgombea hawezi kukwepa kutumia fedha katika
kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura kwenda kupiga kura gharama
hizo nani azibebe.
Katiba ifafanue rushwa ni nini
kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa PROPORTIONAL REPRESENTATION
,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi kuwania majimbo na siyo
wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama chake kupata kura
nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii itasaidia kuondoa
kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze kuwania uongozi.
4.ARDHI
Kwa mwanadamu, kunyang'anywa haki
ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni sawa na kunyanng'anywa haki ya
uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa nguvu wakulima katika suala la
ardhi, na kuwasahau wafugaji.
Wafugaji wamekuwa wakimbizi katika
nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao, ile
ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka kutafuta malisho huku nyuma
imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima au wawekezaji, hili
kwakweli si jambo jema .
Tumeshuhudia migogoro ya ardhi
kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi ningependa katiba hii mpya
impe mfugaji haki katika suala la ardhi kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe,
ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe na hali ya 50,50 situation kati
ya mfugaji na mkulima katika suala zima la umiliki wa ardhi,kikatiba!
No comments:
Post a Comment