Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake wakati wa kusimikwa askofu wa singida KKKTAskofu
mkuu kanisa la KKKT Tanzania, Dk. Alex Malasusa(mwenye fimbo)
akimtambulisha kwa waumini wa kanisa hilo, askofu mteule, Dk. Alex
Mkumbo baadaya kuwekwa wakfu kuwa askofu kanisa hilo,dayosisi ya kati,
sherehe zilizofanyika mjini Singida.
Askofu mkuu kanisa la KKKT Tanzania, Dk. Alex Malasusa(mwenye fimbo)
akimtambulisha kwa waumini wa kanisa hilo, askofu mteule, Dk. Alex
Mkumbo baadaya kuwekwa wakfu kuwa askofu kanisa hilo,dayosisi ya kati,
sherehe zilizofanyika mjini Singida.Askofu
mteule,Dk. Alex Mkumbo wa kanisa la KKKT Dayosisi ya kati, Singida
(Mwenye fimbo), akiwa na askofu Martin Shao wa dayosisi ya
kaskazini(Kilimanjaro) aliyesimama kushoto na askofu Charle Mjema wa
dayosisis ya Pare,(kulia),akiwa ameshikilia fimbo yake ya uaskofu baada
ya kuwekwa wakfu jana mbeleya Rais Jakaya
Kikwete. Baaadhi ya wachungaji kutoka sharika zote kanisa la KKKT Dayosisi ya kati waliohudhuria sherehe hizo.
Singida
Januari 06,2013.
RAISJakaya Kikwete ameyataka madhehebu
ya dini kurejesha utaratibu wa zamani wa kukutana kujadili mahusiano
yao ili kuepuka uhasama wa kidini, unaoHATARISHA amani nchini.
Dk. Kikwete alisema hayo kwenye ibada
ya kumweka wakfu, askofu mteule wa kanisa la KKKT- Dayosisi
kati-Singida, mchungaji Dkt Alex Mkumbo, iliyofanyika makao makuu ya
kanisa hilo, usharika wa Imanuel, Singida mjini.
Alisema, masuala ya udini hapo siku za
nyuma hayakuwepo hapa nchini kutokana na viongozi wa madhehebu ya dini
kukutana na kumaliza tofauti zao mapema,lakini hivi sasa utamaduni huo
umetoweka hali inayoweza kuchangia kutokea kwa machafuko ya udini hapa
nchini.
“Nimeogopeshwa sana na hali ya
kulegalega kwa hali ya amani, utulivu na usalama wa nchi yetu, hususani
kipindi cha mwaka jana…naomba hali hiyo isitokee tena mwaka huu wa
2013,”alisema Dk. Kikwete na kuongeza kuwa.
“Maana hata nilipolazimika kutumia
vyombo vya dola vyenye dhamana ya kutuliza ghasia, bado hali ilikuwa
ngumu…lakini naamini kupitia Misikiti na makanisa mkiendeleakuhubiri
waumini wenu, hali itakuwa shwari,”alisema.
Aidha Dk.Kikwete aliwaomba viongozi wa
dini kuendelea kuwahubiri waumini wao kujiepusha na vurugu za udini,
matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, uvivu,biashara ya ukahaba na
kupiga vita vitendo vya kuomba na kupokea rushwa, ili washiriki vema
kujiletea maendeleo yao.
“Dini na serikali wote tunafanya kazi
ile ile ya maendeleo…wananchi wanahimizwa kujiletea maendeleo na dini
pia inahimiza waumini wake kupata maendeleo,kwa nawaomba tuendelee
kushirikiana pamoja, serikali yangu inaahidi kushirikiana na madhehebu
ya dini,”alisema.
Alisema utaratibu wa zamani wa
viongozi wa dini walikuwa wanatumia kukaa na kujadili maswala mbalimbali
ulikuwa unasaidia kutuliza ghadhabu, kuonya na kufundisha, hali
aliyotaka ufufuliwe na kuhuishwa upya ili kuimarisha amani na utulivu
nchini.
Kwa upande wake askofu mkuu wa kanisa
la KKKT Alex Malasusa alimshukuru Rais Kikwete, kwa kutoa kauli hiyo
inayowahakikishia waumini wamadhehebu yote uhuru wa kuabudu kilamtu na
dini yake.
Dk. Malasusa alimweleza Rais
kuwakanisa litakuwa bega kwa began a serikali,kuhakikisha amani na
utulivu vinaendelea kudumu nchini,licha ya watu wachache kutaka
kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Mapema baada ya kuwekwa wakfu, katika
risala yake askofu Dk. Alex Mkumbo alimwomba Rais Kikwete kusaidia
kurejesha shule ya wasichana ya sekondari Ruruma iliyopo wilaya Iramba,
kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha kuanzishwa kwa dhehebu la
Lutherani, kwenye dayosisi hiyo.
Dk. Mkumbo alimweleza Rais,kwa kuwa
shule hiyo ilichukuliwana na CCM na yeye ndiye mwenyekiti wa taifa wa
chama hicho, kanisa linaiomba ili liweze kuweka mambo mengi muhimu kwa
ukumbusho wa KKKT Dayosisi ya kati.
Hata hivyo katika majibu yake, Rais
aliwataka viongozi wa kanisa hilo kukutana na wenzano viongozi wa mkoa
Singida, ili kumaliza kabisa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment