Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akimkabidhi Bwana Antoine Peigney, jarida lenye kumbukumbu
mbalimbali za kazi zinazofanywa na taasisi ya WAMA mara baaba ya
kufanya mazungumzo na kiongozi huyo wa Red Cross nchini Ufaransa, jana.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa
Uendeshaji na Uhusiano wa Kimataifa wa Shirika la Red Cross la Ufaransa
Bwana Antoine Peigney (wa pili kushoto) kwenye makao Makuu ya Shirika
hilo jijini Paris Ufaransa jana. Mama Salma yuko nchini Ufaransa
akiambatana na Rais Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu ya
kiserikali,
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania
wanaoishi nchini Ufaransa mara tu baada ya Rais Jakaya Kikwete
kuzungumza na Watanzania hao kwenye ukumbi wa hoteli ya Le Meurice
jijini Paris, jana. Picha na John Lukuwi
**************************
**************************
*NI MUHIMU WATOTO WAKAPEWA CHANJO KWA WAKATI
Na Anna Nkinda – Paris
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete amesisitiza umuhimu wa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano kupewa chanjo kwa wakati, chakula chenye virutubisho na
kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwatunza kwa kufanya hivyo nchi itakuwa inapanda mbegu nzuri na baada ya miaka michache taifa litakuwa na watoto wenye afya bora.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ameyasema hayo
jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu la
nchini Ufaransa ambalo licha ya kutoa huduma mbalimbali za dharula pia
linatoa huduma za afya kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Mwenyekiti huyo wa WAMA
alisema kuwa ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano Serikali kwa kushirikiana na shirika la GAVI Alliance kupitia
wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa chanjo ya kuzuia magonjwa ya
homa ya vichomi na uti wa mgongo nchini Tanzania.
“Taasisi ya WAMA imekuwa ikitoa vifaa tiba inavyochangiwa na wadau mbalimbali katika
hospitali, vituo vya afya na Zahanati ambazo zimekuwa na upungufu
mkubwa wa vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vitanda vya
kulalia wagonjwa, mashine za kupumulia watoto wanaozaliwa wakiwa na
matatizo.
Pia kwa kushirikiana na shirika la AMREF International taasisi ya hii imetoa mafunzo kwa manesi ambao wameweza kuwaelimisha watoto wa kike walioko mashuleni jinsi ya kujiepusha na mimba za utotoni”, alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Uhusiano na Oparesheni za Kimataifa za Shirika hilo
Antoine Peigney alisema kuwa shirika hilo linafanya kazi za kukabiliana
na majanga katika nchi 30 Duniani na limeajiri wafanyakazi 17000 pia watu 20000 kutoka nchi hizo wanafanya kazi za kujitolea.
Alisema kuwa Shirika
hilo limekuwa likilisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania pale
lilipoombwa kutoa msaada na kutoa mfano mwaka 2004,
2006 na 2009 lilitoa msaada katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na
mwaka 2011 katika mkoa wa Manyara hivyo basi watafurahi zaidi kama
watapata nafasi ya kufanya kazi na taasisi ya WAMA ili waweze kuwasaidia
watanzania.
Mama Kikwete ameambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Ufaransa kwa ajili ya mwaliko wa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
No comments:
Post a Comment