Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa
jijini Harare, walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo yaliyofanyika jana jijini Harare Zimbwabwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akizungumza jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati wakiwa Ikulu
ya nchi hiyo jijini Harare, jana baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dkt. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare Zimbabwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kushoto) akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe (kulia)
alipomtembelea Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt. Landa John Nkoma, kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati akiondoka
Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais***************************
MAKAMU
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL
AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAZISHI YA MAKAMU WA RAIS WA ZIMBABWE HAYATI
LANDA JOHN NKOMO
HARARE: JANUARI 21, 2012
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
ameiwakilisha Tanzania katika mazishi ya mpigania uhuru na mwanaukombozi
wa Afrika Komredi Landa John Nkomo yaliyofanyika jijini Harare katika
Makaburi ya Mashujaa wa Zimbabwe, jana Januari 21, 2013. Komredi Nkomo
hadi anafikia mauti alikuwa Makamu wa Rais was Zimbabwe na Makamu
Mwenyekiti wa Chama kilichopigania uhuru wa Zimbabwe ZANU-PF Kilicho
chini ya Rais Robert Mugabe.
Makamu
wa Rais Nkomo alifariki Januari 17, 2013 nchini Afrika Kusini
alikopelekwa kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Kansa kwa
miaka kadhaa na alifariki katika hospitali ya Mtakatifu Anne akiwa na
umri wa miaka 79. Katika mazishi ya shujaa Nkomo yaliyofanyika jana na
kuongozwa na Rais Mugabe pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Afrika
Kusini, Zambia, Botswana na Namibia. Maelfu ya wananchi wa Zimbabwe
walihudhuria mazishi hayo huku wakionekana kuguswa na msiba huo mkubwa,
hali iliyowafanya kutokuondoka katika eneo la mazishi hata pale mvua
ilipokuwa ikinyesha.
Rais
Mugabe wakati akilihutubia taifa alisema, Hayati Nkomo alikuwa mfano
thabiti wa amani katika Afrika na hata wakati anapelekwa Afrika Kusini
kutibiwa kabla ya mauti kumfika, alikuwa kinara katika mazungumzo ya
kufikia mkataba wa Makubaliano ya vyama vya siasa juu ya Katiba
itakayotumika kwa jili ya uchaguzi mkuu ujao nchini Zimbabwe,
makubaliano yaliyopitishwa mapema juma lililopita.
Akizungumza
na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal Ikulu jijini Harare, Rais
Mugabe aliishukuru Tanzania kwa kuwa mshirika na ndugu wa karibu katika
hali zote za maisha ya wananchi wa Zimbabwe na akafafanua kuwa udugu
katika nchi hizi ni wa kutukuka na unatakiwa kulindwa na kuenziwa kwa
vizazi vingi vijavyo.
“Mheshimiwa
Makamu, natumia nafasi hii kukuomba ufikishe salamu zangu kwa Rais
Kikwete. Sisi tumefarijika sana kwa ujio wako hapa. Marehemu Nkomo
alikuwa kiongozi madhubuti katika nchi yetu na sasa ametutoka.
Kilichobaki kwetu ni kuendelea na kazi za kuijenga nchi yetu kwa misingi
ya kuthamini amani,” alisema Rais Mugabe.
Katika
ziara hiyo fupi, Mheshimiwa Makamu wa Rais licha ya kuhudhuria mazishi
ya Hayati Nkomo, pia alipata fursa ya kumtembelea Rais Mugabe ofisini
kwake Ikulu jijini Harare na kisha kukutana na baadhi ya Watanzania
waishio Zimbabwe katika makazi ya Balozi wa Tanzania. Katika maelezo
mafupi aliyoyatoa kwa wananchi wa Tanzania waishio Zimbabwe, Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliwataka kujiuliza kuhusu mambo yapi wanaona ni muhimu
na bora kwa kuutangaza utanzania na Mtanzania na kuwataka kuyatumia hayo
hasa sasa wakati tunapoendelea na mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili
yawe chachu ya uzalendo na taswira kwa kila mtanzania kama yalivyo
mataifa mengine.
Watanzania
hao pia waliitaka serikali ya awamu ya nne kuwaelimisha wananchi wa
Mtwara kuhusu umuhimu wa gesi kutumika kwa maendeleo ya taifa na
wakamuomba Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwaelimisha wananchi hao akifanua
pia vyanzo vingine vya gesi vilivyopo nchini, hali inayoweza kuwafanya
watambue kuwa gesi haiku Mtwara pekee.
Kwa
upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais akieleza kuhusu hoja hii alieleza
kuwa, nchi iko katika kipindi cha kuandaa sera ya gesi na mafuta na sera
hiyo ikikamilika wananchi watakuwa na kipindi cha kutazama kama
inalenga kuwanufaisha lakini sasa hivi, wananchi wanapaswa kuwa watulivu
kwa kuwa sera hiyo itazingatia maslahi ya wananchi wote wa Tanzania na
maeneo yote ambapo gesi na mafuta vitapatikana.
.
Makamu
wa Rais na Msafara wake wameondoka hapa leo Jumanne na kurejea nchini
Tanzania tayari kuendelea na shughuli nyingine za kitaifa.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Januari 22, 2012
No comments:
Post a Comment