Mwanahabari wa RFI Kiswahili na Bonesha FM nchini
Burundi, Hassan Ruvakuki
|
Mahakama kuu ya Gitega nchini Burundi, leo imetoa hukumu ya kifungo
cha miaka mitatu dhidi ya Mwanahabari wa Radio Bonesha FM na Ripota wa
RFIKiswahili Bw Hassan Ruvakuki
Mawakili wa Ruvakuki wamesema watakata Rufaa, wakionesha kutoridhishwa na humukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo.
Chama cha Waandishi wa Habari nchini Burundi UBJ kimelaani vikali hukumu
hiyo kikisema kuwa Hassan Ruvakuki hana hatia na hastahili kifungo
hicho.
Wakati Rufaa hiyo inaendelea mwaka jana, Mwendesha mashtaka wa Serikali
alisema kuwal, Hassan Ruvakuki alikwenda nchini Tanzania jirani na mpaka
wa Burundi ambapo alikutana na Waasi na kufanya Mahojiano nao na kusema
kuwa hicho ni kitendo cha uhaini.
Hassan Ruvakuki na Mawakili wake walibainisha mahakamani kuwa alikwenda
kufanya mahojiano na waasi ikiwa ni sehemu ya kazi za kawaida kwa
Mwanahabari.
Baadhi ya Raia waliozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France
International wameeleza juu ya matumaini yao kuwa Hassan Ruvakuki
ataachwa huru kufuatia mbinyo uliotolewa na Wafadhili wa nje wa Burundi
Mwaka jana.
Hassan Ruvakuki na wenzake walikamatwa na kufungwa mwishoni mwa mwaka
2011, na mara zote mahakamani kumekuwa na mvutano ambapo mwendesha
mashtaka wa serikali alishindwa kuthitisha Mashtaka kwa Vielelezo.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment