Na: Fredy Azzah
RAIS
Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea kufedheheshwa kwake
na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau wa maendeleo wa
Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na mihadhara. Mkapa
alitaka wakazi hao
kuacha kulumbana na Serikali kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta mwafaka kwa njia ya amani.
Katika
tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana, Mkapa alisema: “Fujo,
vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti ya maendeleo.
“Nikiwa
kama mwana - Mtwara na raia mwema, mpenda nchi, nimefedheheshwa sana na
matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa
wadau wote wa maendeleo ya Mtwara, kusitisha harakati hizi na
maandamano na mihadhara.
“Badala
yake wajipange kukaa pamoja katika meza moja, kupitia historia,
kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake,
hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo. Liwezekanalo leo
lisingoje kesho.”
Mkapa
alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara
inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali
aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya
siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi
wa Serikali.
“Mtafaruku
huu haufai kuachwa na kutishia usalama, mipango ya maendeleo siyo siri,
mikakati na mbinu za utekelezaji wake siyo siri,” alisema Mkapa na
kuongeza:
“Maelezo
yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo
rasilimali zinawanufaisha wananchi wa eneo zilimo na taifa zima.”
Mkapa alisema hali hiyo ni tishio kwa wawekezaji wa ndani na nje, kwani mara zote hawapendi vurugu, fujo na vitisho.
Kauli hiyo ya Mkapa imekuja siku kadhaa tangu kuwapo kwa maandamano na vurugu zinazofanywa na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya Mkapa imekuja siku kadhaa tangu kuwapo kwa maandamano na vurugu zinazofanywa na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Tayari
viongozi kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete wametoa tamko juu ya suala
hilo wakionya kuwa halikubaliki kwa kuwa rasilimali hiyo si kwa ajili ya
wana Mtwara pekee.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyalaani maandamano
hayo akisema walioyaandaa wamelenga kuigawa nchi vipandevipande, Chadema
kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kumbana waziri huyo ili aondoe udhaifu
uliopo katika sekta ya nishati.
Desemba
mwaka huu, maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga
uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka hapa kwenda
Dar es Salaam.
Maandamano
hayo yaliyoratibiwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Sau, Tanzania
Labour Party (TLP), APPT- Maendeleo, ADC, UDP na DP yakishirikisha
wananchi wa wilaya za mkoa huo, zikiwamo Tandahimba na Newala yalianzia
katika Kijiji cha Mtawanya hadi Mtwara Mjini kupitia barabara ya kwenda
Msimbati eneo ambako gesi asilia inapatikana.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment