Wakaazi wa Bo'o wamesema wingu jeusi limetanda katika kijiji chao kidogo
kutoka washukiwa watatu wa al-Shabaab waliokuwa na silaha kuwapiga
risasi wanawake waliokuwa wakitoka kwenye sherehe za harusi wiki
iliyopita.
Al-Shabaab imeweka sheria kali kuhusiana
na sherehe za harusi ambazo zinajumuisha kupiga marufuku mabibi harusi
kutovaa vazi la harusi la utamaduni wa Somalia. [Yasuyoshi Chiba/AFP]
Sherehe hiyo iliadhimishwa kitamaduni kuweka ishara ya siku saba za ndoa na ilihudhuriwa na wanawake tu.
"Ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu na rafiki wa maharusi hao, kama
inavyopaswa kufanyika wakati kunapokuwa na harusi, na hapakuwa na
matatizo [na al-Shabaab hadi shambulio hilo]," alisema Ugas Hirey,
mkaazi wa Bo'o mwenye umri wa miaka 35. "Hatuwezi kutambua
kilichobadilisha; tulishtushwa na mlio wa risasi na matokeo yake
mabaya."
Al-Shabaab wanadhibiti kijiji hicho kilicho kilometa 30 kutoka mji mkuu
wa Hiran wa Beledweyne, ambao ulikombolewa na vikosi shirika mwezi
Disemba 2011 na kutokea wakati huo wamekuwa wakikataa waziwazi
mashambulio kadhaa yaliyofanywa na kikundi hicho kukomboa jiji hilo.
Kwa mujibu wa mzee wa kabila Jama Ahmed mshambuliaji huyo anasadikiwa
kuwa na umri kati ya miaka 16 na 19. Alisema walisubiri sherehe hizo
kumalizika na kumpiga risasi mwanamke walipokuwa wakiondoka eneo la
sherehe, wakamuua shangazi wa bwana harusi na kuwajeruhi wanawake
wengine wawili.
Waathirika waliojeruhiwa walikimbizwa mara moja katika Hospitali ya Beledweyne kwa matibabu.
Mmoja wa waathirika alipoteza damu nyingi na alikuwa na hali mbaya sana
alipofikishwa hospitali, mkurugenzi wa Hospitali ya Beledweyne Ahmed
Khalif aliiambia Sabahi. Wanawake wote wawili kwa sasa hali zao
zinaimarika na wanapata matibabu muhimu.
Wakazi wanatii sheria zote za al-Shabaab
Wakazi waliiambia Sabahi walikuwa wanahofia usalama wao na hawaelewi ni
kwa nini al-Shabaab walilenga sherehe ya harusi kwa kuwa ilifanyika kwa
mujibu wa sheria za wanamgambo. Wengi walikataa kuzungumza kwa
kurekodiwa kwa kuhofia ulipizaji kisasi kutoka kikundi cha wanamgambo.
Katika sheria za al-Shabaab, maharusi wanakatazwa kuvaa nguo za
utamaduni wa Somalia, gauni jeupe lenye mkono mmoja lililozungushiwa
kashida nyekundu na kahawia. Badala yake, wanawake lazima wavae sketi
nyeusi ndefu iliyoshonwa kwa kutumia kitambaa kizito na blauzi ndefu
inayofunika kuanzia vichwani kwao hadi chini ya kiuno. Zaidi ya hayo,
mwanaume na mwanamke lazima watenganishwe, muziki wowote umepigwa
marufuku, na msafara wa harusi usiwe na magari zaidi ya matatu.
Mzee wa kabila alisema hakuna mtu aliyekiuka sheria zilizowekwa, na shambulizi halikuwa na sababu kabisa.
Ahmed alisema wakazi wenyeji wanatambua sheria kali ambazo al-Shabaab
wameziweka kwa raia kuhusiana na mikusanyiko na sherehe, na kila mtu
amekuwa mwangalifu kuzifuata kwa kuwa kikundi cha wanamgambo
kinalidhibiti eneo kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Wageni walighani mkarara ulioitwa "buraanbur" kusherehekea bibi harusi,
bwana harusi na familia zao. Mkarara huo haukuhusisha jambo lolote
lililozuiliwa na al-Shabaab, alisema.
"Tukio la Bo'o limewabainisha watu wanaoishi katika mkoa wa Hiran na
kuwaacha wakishangaa kwa sababu al-Shabaab wameibadilisha siku
iliyopaswa kuwa ya kusherehekea na kuwa siku ya majonzi," alisema Ahmed.
"Inaonyesha al-Shabaab hawana huruma kwa wale wanaoishi chini ya sheria
yao."
Wazee wa kabila kimila walijaribu kusuluhisha ugomvi miongoni mwa
wananchi ikiwa ni pamoja na matukio ya vurugu kama hii. Hata hivyo,
Ahmed alisema haina maana kushirikishwa katika suala hili kwa sababu
wapiganaji wa al-Shabaab hawaheshimu wajibu wa wazee na hawatakuwa
wasikivu kama watawafuata.
"Hatuwezi kuwavumilia kuendelea na mambo yao mabaya wanayoyafanya kwa
sababu tuna wasiwasi yatasababisha uharibifu zaidi," alisema.
Hii sio mara ya kwanza kwa wanamgambo wa al-Shabaab kushambulia sherehe
za harusi. Hivi karibuni, sherehe ya harusi ilishambuliwa mwezi wa
Disemba katika kijiji cha Qurod karibu na El Bur, na kuua watu wanne na
kuwajeruhi wengine tisa, kwa mujibu wa Hiiraan Online ya Somalia.
Al-Shabaab bado hawajasema lolote kuhusiana na shambulio la harusi ya Bo'o.
No comments:
Post a Comment