MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Januari 25 mwaka huu,
itasikiliza ombi la kupatiwa dhamana limsanii wa Filamu nchini,
Elizabeth Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia Na.
125/2012 msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Ombi hilo la dhamana ambalo tayari limeishapangiwa Jaji Zainabu
Mruke kuanza kulisikiliza ombi hilo wakati bado kesi yake ya msingi ya
kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa,
limewasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa Lulu ambaye anaishi
gereza la Segerea ,na wake Peter Kibatara,Kenned Fungamtama ,Fulgence
Massawe.
Kwa mujibu wa hati ya ombi hilo la dhamana,mawakili wa Lulu
wameonyesha wamewasilisha ombi lao hilo wameliwasilisha chini ya kifungu
cha 148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002 .
“Lulu ni mtu maarufu nchini, anaiomba mahakama hii impatie dhamana
na yupo tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayo tajwa na mahakama
hii, na anaahidi kuyatimiza masharti hayo wakati akisubiri kesi yake ya
msingi ya kuua bila kukusudia itakapopangiwa tarehe ya kuanza
kusikilizwa katika mahakama yako tukufu”alidai Wakili Kibatara katika
hati hiyo.
Desemba 21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na
kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa
mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake
kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta
jumla ya mashahidi tisa.
No comments:
Post a Comment