Pages


Photobucket

Friday, January 11, 2013

Filikunjombe aitaka serikali kuwajibika liganga na mchuchuma


444b 442b8

Na Bazil Makungu Ludewa
MBUNGE wa Ludewa katika Mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe ameitaka
serikali ya Tanzania kutimiza wajibu zake kwa kutekeleza mkataba na
makubaliano yaliyoingiwa kati yake na wawekezaji walioko Liganga na
Mchuchuma ili kuwezesha miradi hiyo kuanza kwa wakati.
Filikunjombe aliyasema hayo jana alipotembelea maeneo ya uwekezaji ya
Liganga na Mchuchuma kujionea mwenyewe hatua iliyofikiwa na wawekezaji
hao na kupokea changamoto zinazodhoofisha kasi ya kuanza utekelezaji
wa machimbo hayo yanayosubiriwa na kwa hamu na watanzania wengi.

’’’’’ Nimefurahishwa na kasi waliyonayo wawekezaji lakini
nimesikitishwa na kasi ndogo ya serikali katika kutekeleza yale
yaliyomo kwenye mkataba ikiwa ni pamoja na kutengeneza barabara
inayotoka njombe hadi yalipo machimbo ili kupitisha magari na mitambo
mikubwa’’’’’ alilalamika Filikunjombe
HUANG DAXIONG afisa mtendaji wa kampuni ya Tanzania China
International Minerals Resouces Limited iliyoundwa kwa ubia kati ya
Tanzania na china akitoa taarifa kwa mbunge huyo alisema kasi ya
kuanza kwa machimbo ya makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha Liganga
kunadhoofishwa serikali kushindwa kutimiza masharti yaliyomo ndani ya
mkataba.
Daxiong aliongeza kuwa wao wanafanyakazi usiku na mchana kulingana
mkataba lakini wanashindwa kwa sababu mitambo mikubwa inashindwa
kufika eneo la mradi kutokana na serikali ya Tanzania kushindwa
kutengeneza barabara za kupitisha mitambo hiyo.
‘’’’’ miradi hii itashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na serikali
kutotimiza masharti yaliyomo ndani ya mkataba, sisi tunakwenda na
wakati lakini tunakumbana na changamoto ambazo mtatuzi ni Serikali ya
Jamuhuri ya Tanzania hivyo tunakuomba mbunge utusaidie.’’’’ Alisema
Huang
Bw.Daxiong aliyataja makubaliano ya kampuni yake na Serikali kupitia
shirika la Taifa la maendeleo(NDC) kuwa ni pamoja na upanuzi wa
barabara kuu kutoka Njombe hadi Mchuchuma ambako ndiko kwenye makaa ya
mawe.
Alisema wanashindwa kupitisha mitambo ya kufanyia kazi kutokana na
barabara hiyo kuwa nyembamba na madaraja madogo ambapo ni vigumu
kupitisha gari zenye tani kubwa katika barabara za wilaya ya Ludewa.
“makubaliano yetu na Serikali ilikuwa ni upanuzi wa barabara haraka
iwezekanavyo ili tuweze kufanya kazi ambayo inategemea zaidi
kusafirisha mitambo kutoka bandari ya Dar es salaam hadi migodini
lakini sisi tumeshaanza kazi Serikali ya Tanzania bado”,alisema
Daxiong.
Aidha Daxiong akazitaja changamoto nyingine zinazodhoofisha mradi huo
kuwa ni pamoja na urasimu ulioko bandari ya Dar es Salaam katika
kuchukua mitambo yao inayotoka nchini China na ucheleweshaji wa vibari
vya kufanyia kazi.
Bw.Daxiong alisema urasimu huo ulioko Bandarini pamoja na
ucheleweshaji wa vibari umekuwa changamoto kubwa kwao kwani mitambo
mingi bado iko bandarini na haijulikani hatima ya tatizo hilo kwani
muda unazidi kwenda bila mafanikio.
Alisema suala la vibari lilianza kushughurikiwa kabla ya kusaini
mkataba lakini kumekuwa na urasimu mkubwa ambao unawakatisha tamaa
wawekezaji hao katika kuifanya kazi hiyo ya uanzishaji wa mgodi kwa
wakati muafaka kama walivyotarajia.
Daxiong alimuomba Filikunjombe kuishawishi Serikali ili kuharakisha
vibali vya kazi,upanuzi wa barabara na kuondoa urasimu bandarini ili
waweze kuondoa mizigo yao haraka pindi inapofika bandarini hapo.
Filikunjombe aliahidi kufuatilia malalamiko hayo lakini akaitaka
kampuni hiyo kutokatishwa tamaa na mambo hayo kwani Serikali iko
makini ingawa kuna watu wachache wanaozembea kwa maslahi binafsi.
Mkataba unaonesha kuwa kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Limited
itawekeza dola za kimarekani bil 3.0 miradi ya Liganga na Mchuchuma na
kwamba katika awamu ya kwanza uzalishaji umeme kutoka makaa yam awe ya
mchuchuma ni megawati 300 mwaka 2015 na uzalishaji chama cha Liganga
ni tani 500,000 kwa mwaka kuanzia mwaka 2015/16 ambapo awamu ya pili
itakuwa kuzalisha umeme kufikia megawati 600 na chuma kufiki tani m.1
kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment