Zimamoto wakiwakwenye uokoaji katika ukumbi huokatika ajali ya moto iliyotokea
kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Watu wakiwa kwenye simanzi katika ajali ya moto iliyotokea
kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Uhokoaji ukiendelea katika ajali ya moto iliyotokea
kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Raia
wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili
thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea
kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.Maafisa
wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada
ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya
Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto
huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki. Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama
wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima
moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi
kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu
ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama
jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe
iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia,
kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo
mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo. Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa. Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment