Pages


Photobucket

Saturday, May 4, 2013

MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO MCHANA .Tazama PICHA



Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha



Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.




MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodhahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu. Alisema baada  ya  Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio.....Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
 Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya. Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili  yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
 Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

No comments:

Post a Comment