
Jeshi nchini
Nigeria limesema watu hamsini na watano wameuawa huko kaskazini
mashariki mwa Nigeria katika mashambulio yaliyofanywa na wanamgambo wa
kundi la Boko Haram. Taarifa zinasema, wafungwa 105 walitoroshwa katika shambulio hilo mapema alfajiri lililotokea katika jimbo la Bama, Borno. Aidha, mashahidi na jeshi linasema kituo cha polisi cha Bama, majengo ya serikali na kambi za kijeshi ziliteketezwa kwa moto.
No comments:
Post a Comment