Pages


Photobucket

Sunday, May 5, 2013

HALI ILIVYOKUWA JUU YA MLIPUKO KATIKA PAROKIA TEULE YA OLASITI


1. Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Kanisa Katoliki Arusha, Mhashamu Josephat Lous Lebulu na Mwakilishi wa Papa, Nuncio Francisco Montecillo Padillawameondoshwa katika eneo la tukiona kikosi cha ulinzi na usalama.

2. Kikao cha dharura cha ulinzi na usalama kimeafikiana kusitisha shughuli ya leo hadi hapo itakapotangazwa upya.

3. Padre Simon Mtengesi amefunga rasmi ibada kwa sala fupi na kuwaomba watu warejee majumbani mwao.

4. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amefika na kutizama maeneo ya Kanisa, kisha akazungumza kwa kusema kuwa mwakilishi wa Papa alikuwepo Arusha tangu tarehe 2 Mei akitembelea maeneo kadhaa ya mkoa huo, ikiwemo Ngorongoro na leo alikuwa katika kilele cha ziara yake kwa kuzindua Parokia mpya, ndipo mlipuko huo ukatokea na kusababisha shughuli nzima kuahirishwa. Magesa amesema wataalamu wa uchunguzi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wanatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kuungana na kikosi cha Mkoani hapo ili kufanya shughuli ya uchunguzi.

5. Mkuu wa kikosi cha Polisi cha usalama Mkoani Arusha, RPC Kamabda Liberatus Sabas amefika katika eneo husika na kuzungumza akiswma kuwa walipokea taarifa za tukio kwa maelezo kuwa mlipuko ulitokana na kitu cha kurushwa kutoka kwa mtu mmoja aliyefika eneo hilo kwa gari. Hadi sasa Polisi inamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano zaidi na inaomba wananchi wenye taarifa zaidi waziwasilishwa katika vyombo husika.

6. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefika katika eneo na kuzungumza na wananachi. Amesema hili ni tukio la kushitua sana kwa kuwa limetokea kwenye eneo la ibada, wakati misa ikiendelea... (mawasiliano ya redio yamekatika wakati Lema anazingumza. Baada ya muda mtangazaji wa Radio Maria ameomba samahani kuwa kuna mtu alizima swichi. Baadaye mwandishi alimpata Lema akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jashua Nasaari na kuwapa nafasi ya kuzungumza na kutoa ujumbe wao kwa wananchi.)

7. Padre wa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Sombetini katika Jimbo Kuu la Arusha, Moses Mwaniki amewapa pole majeruhi na kuwaomba watu kujitolea kwa maji na vyakula kwa ajili ya kuwajali majeruhi zaidi ya 30 waliolazwa katika hospitali mbalimbali.

---

Mwendo wa kuelekea saa tano adhuhuri ya leo katika Parokia ya Mpya ya Yosefu Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa leo, pametokea mlipuko uliojeruhi watu kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umtookana na kitu ambacho kinasadikika kuwa lilikuwa ni bomu. Hata na hivyo haijafahamika ikiwa ndivyo, lilikuwa ni bomu la kutegwa ama kurushwa kwa mkono. Ni vigumu na mapema sana kuthibitisha kilicholipuka. Tafadhali tuvute subira kwa kuisubiri taarifa ya Polisi.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa. Majeruhi wamepelekwa katika hospitali mbalimbali za mkoa huo kwa matibabu zaidi.

Kwa muda huu, viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Nuncio Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

1 comment:

  1. Mi Lucy Nawapa pole sana majeruhi walioumia katika ajali hiyo pia na hata waumini wote ambao wamekumba na tatizo hilo , mapadri na papa aliyekuwa anatabaruku kigango hicho Mungu awape moyo wa uvumilifu kwani ni kitu cha kisikitisha sana,kweli watu wameacha kumuongopa mungu kabisa hata kanisa unaenda kumuua mwenzako dunia imetekwa na shetani hiyo, Tunauhakika kuwa wakristo tukiugana na kumuomba mungu kwa sala na mfungo hakika hao watu mungu atawaadhibu. AMENI

    ReplyDelete