Pages


Photobucket

Thursday, May 16, 2013

Mgomo wa wafanyakazi 'wanukia' TRL

Chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini  (Trawu),  kimeitaka Serikali kuongeza kiwango cha mishahara kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), vinginevyo kitaisimamisha treni ya abiria maarufu kama treni ya Mwekyembe. Akizungumza kwenye mkutano na wafanyakazi wa TRL jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Trawu Taifa, Erasto Kihwele, alisema kuwa wafanyakazi wamechoshwa na mishahara midogo wanayolipwa kwa miaka 15 sasa bila ya nyongeza.

Kiwhele alisema kuwa ni miaka 15 sasa toka Serikali ilipopandisha mishahara kwa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Sh. 50,000 mpaka 205,000 wakati gharama za maisha zimepanda huku wafanyakazi wa kada nyingine wakiongozewa mishahara kila wakati.
Aliongeza kuwa uongozi wa Trawu umeamua kwenda Dodoma kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa nyongeza ya mishahara ya wafanyakzi wa kampuni hiyo.
“Kwa kweli safari hii tumeamua endapo hawatatupandishia nyongeza ya mishahara kwa asilimia mia moja tutaweka vitendea kazi chini na kuanza mgomo wa nchi nzima ili kuishinikiza Serikali,” alisema.
Alisema wameazimia kwenda Dodoma kuonana na Pinda baada ya kuona Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu wake kushindwa kutatua matatizo yao.

No comments:

Post a Comment