Pages


Photobucket

Tuesday, May 7, 2013

Waziri Mkuu Pinda kukabidhi madawa, kuwafariji wahanga wa mlipuko Arusha


Mahmoud Ahmad Arusha
Waziri mkuu Pinda kukabidhi Madawa yenye thamani ya tsh.16.2 milion kwa Hospitali ya mkoa mount Meru wakati atakapowatembelea wagonjwa walipata majeruhi kwenye muendelezo uliotokea jana wa mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu JosephMfanyakazi eneo La olasiti Nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Akizungumza wakati akitoa Mablanketi kwa niaba ya wizara ya utalii kupitia shirika la hifadhi la taifa (TANAPA)Naibu waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa wizara yake kupitia Tanapa wametoa vifaa hivyo ili kusaidia hospitali hiyo yenye huba wa madawa na vifaa mbali mbali ikiwemo upungufu wa vitanda,madawa na mablanketi ambayo sehemu ya madawa itakabidhiwa jioni na Mh.waziri mkuu kwa niaba ya serekali.

“Kwanza tunatoa pole kwa majeruhi wote waliopatwa na tukio hilo na tunawatakia wapone haraka pili msaada huu tunautoa kwa ajili ya kupunguza upungufu uliotokea kwenye hospitali yetu ntakaa na wenzangu wadau wa utalii tuangalie nini cha kufanya” alisema nyalandu.
Alisema kuwa jumla ya tsh.16.2 milion zitatumika kununulia madawa ambayo ya takabidhiwa jioni na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda..

No comments:

Post a Comment