Pages


Photobucket

Saturday, May 4, 2013

MOURINHO KUHUSU LAMPARD NA JOHN TERRY CHELSEA

imageKocha wa Real Madrid ambaye amevumishwa kuwa karibu kujiunga na Chelsea Jose Mourinho ameazimia kuhakikisha anawabakiza wachezaji wakongwe wa klabu hiyo John Terry na Frank Lampard.
Wachezaji hao wawili ambao ni manahodha wa Chelsea wamekuwa na wakati mgumu chini ya kocha wa Muda Rafael Benitez ambaye amekuwa hawatumii kwenye mechi nyingi huku akiamini kuwa umri wao mkubwa unamaanisha hawawezi kupata nafasi kama walivyokuwa na umri mdogo.
Frank Lampard anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya Chelsea na uongozi wa klabu hiyo umegoma kumuongezea mkataba jambo ambalo mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakilipinga vikali, hata hivyo inasemekana Mourinho ambaye anawaamini sana wachezaji hao amemuagiza mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kuhakikisha Terry na Lampard wanabaki Chelsea kwani wako kwenye mipango yake .
Zaidi ya hapo Mourinho pia anadaiwa kukanusha usajili wa Radamel Falcao ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye mipango ya usajili wa Chelsea pamoja na Xabi Alonso ambaye amehusishwa na usajili wa Chelsea endapo Mourinho atarudi.

No comments:

Post a Comment