Pages


Photobucket

Friday, November 30, 2012

MAADALIZI YA MAHAFALI YA 47 YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) KAMPASI YA DODOMA YAPAMBA MOTO

Hatimaye ile siku ambayo imekuwa ikisubiliwa kwa kipindi kirefu sasa imefika,Ni kuhusu Mahafali ya 47 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma ambayo inatarajiwa kufanyika kesho Tarehe 1/12/2012 siku ya jumamosi.
Kwa siku ya  leo zimekuwepo pilika pilika mbalimbali katika chuo hicho kwa kuwahusisha  wahitimu pamoja na waandaaji  wa Mahafali hiyo.
Katika hatua nyingine HOTEL YA FIFTY SIX ( iliyoko nyuma ya Chuo hicho) ili kudumisha ujirani mwema  Imejitolea  kuwasaidia bure wahitimu hao kutumia kumbi za nje (Eneo la wazi la Hotel hiyo) kwa ajili ya kusherekea Mahafali hayo ingawa kwa yeyote atakayependa kufanya hivyo atalazimika kununua chakula na vinywaji katika Hotel hiyo.
 
    BI. SHADOLLO  WARDEN (KULIA) AKITOA  BAAADHI YA MAELEKEZO 

Mwendesha mashtaka Korea Kusini ajiuzulu

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu, baada ya kuomba msamaha hadharani kushusiana na kashfa kadhaa katika idara yake.
Han Sang-dae alisema matukio hayo, yaliyowahusisha maafisa chini ya usimamizi wake, yaliwashangaza na kuwavunja moyo watu wengi nchini humo.
Katika kisa kimoja, ofisa wa ngazi ya juu ameshtakiwa kwa kupokea rushwa, huku mwingine ameshtakiwa kwa kupunguza adhabu ya mshukiwa fulani na badala yake kuomuomba wawe wapenzi.

Chanzo ni BBC

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. MUHONGO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UJERUMANI



Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes mara alipomtembelea Profesa Muhongo ofisini kwake. Balozi huyo aliongozana na watendaji kutoka kampuni ya Koch Engineering & Construction ya nchini Ujerumani ambao wanania ya kuwekeza katika miradi ya nishati ikiwamo gesi asilia, umeme wa upepo, jua pamoja na kuwekeza katika viwanda vya uzalishaji mbolea.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes ramani ya bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Profesa Muhongo alimueleza mheshimiwa Balozi kuwa Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi katika eneo la Somangafungu.

 Picha na Afisa Habari Wizara ya Nishati na Madini.

VIKOSI VYA USALAMA NCHINI KENYA VYAZUA TAFRANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Na Rajab Ramah, Nairobi
Wasiwasi unaongezeka juu ya uwezo wa vikosi vya usalama vya Kenya kuzuwia vurugu na kujibu matatizo kwa ufanisi huku uchaguzi mkuu ukiwa umebakia miezi mitatu tu, vikundi vya asasi za kiraia vyasema.

Afisa wa Kitengo cha Huduma Maalumu akimpiga teke kijana wa kenya katika kitongoji cha Eastleigh Nairobi hapo tarehe 19 Novemba, siku moja baada ya bomu kulipuka katika basi dogo, lililowaua watu saba. [Na Carl de Souza/AFP]

Tabia za polisi hivi karibuni katika kukabiliana na vitisho vya usalama zimezua hofu na wasiwasi kuliko uhakika miongoni mwa wananchi, kwa mujibu wa Odhiambo Oyoko, mratibu mtendaji wa Kituo cha Uimarishaji Haki na Ulinzi.

"Kila operesheni ya polisi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu huishia katika kukamata watu kwa makundi bila ya kuchagua, ubakaji, uvamizi, au aina nyengine ya vurugu [zinazoelekezwa] kwa watu wasio na hatia. Hili ni kinyume na dhamiri ya kupambana na uhalifu," alisema, akikisudia operesheni za karibuni huko Tana River Delta, Baragoi, Eastleigh na Garissa.

Mwezi wa Septemba, zaidi ya watu 100 waliuawa katika mapambano ya kikabila huko Tana River Delta, wakiwemo maafisa wa polisi tisa, kabla ya vikosi vya usalama kuweza kuidhibiti hali hiyo.

Tarehe 10 Novemba, polisi 42 waliuawa na majambazi huko Baragoi Wilaya ya Samburu katika Mkoa wa Bonde la Ufa. Kutokana na madai kuwa polisi walichukua hatua kwa taratibu katika kushughulikia mzozo huo, Rais wa Kenya Mwai Kibaki alipeleka Vikosi vya Ulinzi vya Kenya katika eneo hilo ili kuwasaidia polisi.

Siku tisa baadaye, kuuliwa kwa risasi askari watatu wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya huko Garissa kulipelekea maafisa wa jeshi kulipiza kisasi kwa jamii katika ghasia za utumiaji nguvu.

Kukosekana na uratibu, polisi wenye zana hafifu

Simiyu Werunga, mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Masomo ya Usalama na Mikakati kilichoko Nairobi, alisema kuwa hadithi kama hizo zimekuwa za kawaida sana katika miezi ya karibuni, na mara nyingi mashambulizi ya kigaidi ndio huifanya hali kuwa mbaya zaidi.

Werunga, kapteni wa jeshi mstaafu, alisema kukosekana kwa uratibu miongoni mwa vyombo vya usalama ndio sababu ya kuendelea kukosekana kwa usalama.

"Tumeona kesi ambapo jeshi au Kitengo cha Huduma Maalumu kinapelekwa ili kushughulikia kutokuwepo kwa usalama, ambapo polisi wa kawaida wangeweza kuidhibiti hali hiyo," aliiambia Sabahi. "Hali hii unazua mtafaruku na kuleta hofu kwa umma."

Alisema kuwa hatua madhubuti za usalama zinapasa kuchukuliwa mara moja ili kuwahakikishia Wakenya uchaguzi wa amani na salama hapo tarehe 4 Machi 2013.

"Kuna haja ya kuwa na mkabala ulioratibiwa vyema ambao utavijumuisha vyombo vyote katika kugundua na kushughulikia uhalifu," alisema. "Hii inaweza kutokea iwapo vitengo vyote vya polisi vimewekwa chini ya uongozi mmoja wa mkoa."

Polisi wanapaswa kuacha kutoa adhabu za kubambikiza kwa wenyeji wa maeneo ya uhalifu, alisema. Badala yake, wanatakiwa wajenge mahusiano na jamii ambazo badala yake zinasaidia kutoa intelijensia yenye thamani ambayo itapelekea kukamatwa kwa wahalifu.

Alisema kuwa ghasia za karibuni za askari huko Garissa na operesheni zisizochagua zinazowalenga watu wa jamii ya Wasomali katika kitongoji cha Eistleigh huko Nairobi kumemomonyoa mafungamano na uaminifu baina ya polisi na jamii.

Philip Onguje, mratibu wa Jukwaa la Mageuzi ya Usalama, kikundi cha kijamii ambacho kinatetea mageuzi ya sekta ya usalama nchini Kenya, aliiambia Sabahi kuwa polisi wana zana hafifu za kuweza kushughulikia miendo inayoibuka ya uhalifu.

Alisema iko haja ya kuwafunza upya polisi katika kudhbiti mizozo ya uchaguzi na udhibiti wa makundi ili kuepuka matumizi ya nguvu kupita kiasi au operesheni za usalama zinazopendelea au kuonea upande mmoja.

Onguje alisema kuwa utafiti uliofanywa na jumuiya yake mwezi uliopita zilionesha kuwa hakuna hata kituo kimoja cha polisi nchini kati ya vituo 456 kina vifaa vya usalama au uwezo wa kupambana na uhalifu.

"Lilipaswa kuwa suala la kumshughulisha kila Mkenya," alisema. "Lazima sote tushinikize kwa kuwepo kwa marekebisho, kuvipatia vituo vya polisi vifaa na kuajiri maafisa wengi zaidi wa polisi ndani ya miezi michache iliyobakia ili waweze kuhakikisha uchaguzi wa salama mwaka ujao."

Serikali inashughulikia kasoro
Kaimu Katibu Mkuu wa Usalama wa Ndani Mutea Iringo aliiambia Sabahi kuwa serikali inashughulikia wasiwasi huu na inao udhibiti wa usalama wa nchi.

Alisema kuwa serikali inakusudia kuwapa mafunzo maafisa polisi 7,000 ambao watapelekwa nchini kote ifikapo mwezi Januari ili kuliongezea nguvu jeshi la polisi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2013.

"Pia tutawapa mafunzo maafisa wote kwa uchaguzi, haki za binadamu na masuala mengine ya kipolisi na tunawahakikishia Wakenya kuwa katika uchaguzi ujao tutalindwa vyema na maafisa wetu," Iringo alisema.

Serikali pia imo katika mchakato wa kumajiri Inspekta Jenerali wa polisi katika juhudi za kuhamisha uongozi na kusaidia kupanga upya jeshi zima ili liweze kukabiliana na uhalifu kwa ufanisi, alisema.

Mitt Romney, President Obama's Private Lunch at the White House

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA KANU GIDEON MOI JIJINI NAIROBI



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha KANU Mhe Gideon Moi aliyemtembelea jana  Novemba 29, 2012 katika hoteli ya Nairobi Serena jijini Nairobi

HAWA NI BAADHI YA MASTAA WA BONGO WALIOKWENDA KUMZIKA SHARO MILLIONEA


 Wema Sepetu (kulia) na Jack wa Chuz wakishiriki mazishi ya marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea'.
 Yusuf Mlela (kulia) na Sajuki nao wakishiriki mazishi ya Sharo Milionea wilayani Muheza mkoani Tanga jana.…
 ...Ray Kigosi naye alikuwepo.
 Swaiba wa marehemu Sharo Milionea, mzee Majuto akiongea machache wakati wa mazishi hayo.
 Msanii H- Baba akishiriki kumzika marehemu Sharo MilioneaJUZI
 endelea kutembelea blog ya ujanatz
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akimkabidhi Rais wa Shirikisho
la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba ubani wa Airtel kwa ajili ya msiba wa marehemu Sharo Milionea.

HIVI NDIVYO BASATA ILIVYO OMBOLEZA VIFO VYA WASANII




                                                                        John Maganga
Mlopelo
 
Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za misiba ya wasanii watatu wa tasnia ya filamu na muziki nchini.
“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya vifo hivi vya wasanii hawa John Mganga, Mlopelo na Hussein Mkeity a.k.a Sharo Milionea ambao mchango wao unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo waliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia za marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na wapendwa wetu.
Tunaomba mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu. Baraza liko pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.


Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA 30/11/2012













Polisi Wajeruhi Kwa Mabomu Dar


  Na: Joseph Zablon Dar
POLISI wamewajeruhi watu watatu kwa mabomu, mmoja kati yao akiwa katika hali mbaya katika matukio mawili tofauti ya kusambaratisha mikusanyiko iliyotokea Tegeta, Dar es Salaam na Rufiji mkoani Pwani.

Aliyejeruhiwa vibaya ametambuliwa kuwa mkazi wa Tegeta, John Paul ambaye baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala na baadaye Muhimbili.Tukio la Tegeta lilitokea wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wananchi waliokuwa wakipinga operesheni ya kuwaondoa katika hifadhi ya barabara katika eneo hilo saa nne asubuhi baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya Mwankinga wakiwa na polisi waliyolikamata gari la mkazi mmoja wa eneo hilo.Hali hiyo ilizua ubishi na baadaye vurugu baada ya wakazi hao kutaka gari hilo lisichukuliwe na polisi.

Vurugu hizo ziliwafanya polisi kutumia nguvu kuwatawanya wakazi hao, kazi ambayo hata hivyo, haikuwa rahisi kwani nao walikuwa wakijibu kwa kuwarushia mawe na fimbo, hali iliyodumu kwa saa kadhaa na kufanya eneo hilo kugeuka uwanja wa mapambano kusababisha maduka kufungwa na mali kuharibiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Chales Kenyela alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kueleza kuwa, kijana huyo alijeruhiwa shavuni na kitu ambacho bado hakijafahamika na kupelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Kamanda Kenyela alisema kuwa, polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Alisema awali, wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa na polisi, walifika eneo hilo na kuanza operesheni ya kuondoa magari.

“Walipokamata gari la mmoja wa wakazi wa eneo hilo wananchi hao walipinga na kuanza kuwafanyia vurugu polisi ambao walijibu mapigo kwa kupiga mabomu ya machozi na kuwatawanya. Kijana huyo alionekana baadaye akiwa amejeruhiwa na kupelekwa Mwananyamala,” alisema. Katibu wa Afya katika Hospitali ya Mwananyamala, Edwin Bisakala alithibitisha kupokewa kwa majeruhi huyo na kudai kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa alijeruhiwa kwa bomu.
Bisakala alisema hali ya majeruhi huyo ilikuwa mbaya na uongozi wa hospitali ulilazimika kumpeleka Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.Mmoja wa mashuhuda wa vurugu hizo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisimulia jinsi eneo hilo lilivyokuwa: “Polisi wanarusha mabomu na wananchi wanawarushia mawe, ilikuwa tafrani kubwa hapa.”
Alisema hali hiyo iliwafanya polisi wajibu kwa kupiga risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi hali iliyozua taharuki na baada ya watu kutawanyika, kijana huyo alionekana akiwa ameanguka chini, huku damu zikimvuja.

Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi alithibitisha kufikishwa kwa kijana huyo katika hospitali hiyo akimtaja kwa jina la John Massawe. Alisema alikuwa amejeruhiwa vibaya kichwani.

Kibonzo ITV

Thursday, November 29, 2012

MNYIKA: HATUWEZI KUTOA ORODHA YA MAJINA YA VIGOGO WALIOFICHA FEDHA USWISS


MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha ya vigogo walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina hayo kama Serikali inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi ambayo ilitajwa Mwembe Yanga bado haijashughulikiwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara jijini Mwanza, Mnyika alisema kwamba kama Serikali ya CCM inasisitiza kutaka majina ya walioficha fedha huko Uswiss yatajwe, wanapaswa kusimama na kueleza ile orodha ya mafisadi ambayo Chadema waliitaja pale Mwembe Yanga imefanyiwa kazi gani.
“Watu wanapotutaka tutaje majina, na sisi tunawambia kwanza wasimame na kutueleza ile ‘list’ (orodha) ya mafisadi ambayo tuliitaja kwa majina wameishughulikia vipi?” alihoji Mnyika na kuongeza kwamba wanajua jinsi ambavyo CCM wanalivyonufaika na ufisadi kupitia Kampuni ya Kagoda jambo ambalo linadhihirisha kuwa haiwezi kuwa rahisi kwao kushughulika na vita ya ufisadi.
Alisisitiza kuwa wanaotaka majina yatajwe wanayo ajenda yao na wao wameshaifahamu hivyo hawatashughulika nayo na kusema ukifika wakati ambao wao wanautambua wataweka kila kitu nje, lakini siyo kwa kushinikizwa na Serikali ya CCM.
“Tunajua serikali hii inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi haina dhamira ya kushughulika na ufisadi, na hili ndilo litakalowaondoa madarakani,” alifafanua.
Hata hivyo mkutano huo uliingia dosari wakati Mnyika akiendelea kuhutubia ambapo mawe yalianza kurushwa na vijana wanaodaiwa kuwa ni vijana wa Diwani wa Kata ya Kitangiri kwa tiketi ya Chadema, Henry Matata aliyevuliwa uanachama.

Kutokana hali hiyo vijana wa Chadema walizungumza katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa vijana wawili ambao walishambuliwa na kueleza na kunusuriwa na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje aliyeita polisi na kuwaomba waache kuwashambulia.
Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Wenje alieleza wananchi kuwa katika mkakati wake wa kuboresha elimu ya msingi na sekondari amefanikiwa kutengeneza madawati mengine 400 baada ya madawati ya awali 500 kugawiwa katika shule.
Alisema madawati hayo yatagawanywa kwa shule 30 za wilaya ya Nyamagana na kubainisha kwamba kutokana na madaati ya awali 500 kutolewa bila utaratibu na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,Wilson Kabwe hivyo madawati haya alieleza kuwa yatasambazwa na madiwani wa Chadema katika shule pamoja na katibu wa ofisi yake ili kuhakikisha yanafika katika shule husika iliyopangwa.
Mwananchi

RAIS KIKWETE NA VIONGOZI WENGINE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA - NAMANGA - ATHI RIVER


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Kenya,Mh. Batilda – Salha Burhan.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012.Rais Kikwete yupo nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Wengine Pichani ni Rais wa Kenya,Mh. Mwai Kibaki (katikati) na Rais wa Burundi,Mh. Nkurunzinzah.

Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la nchini Kenya wakiwa kwenye Sherehe hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipata maelezo ya Barabara hiyo itakavyokuwa kutoka kwa Injinia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River.
 
*******************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************

Jengo La Jumuiya Ya Afrika Mashariki Nalo  Lazinduliwa

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
 Mfano wa  jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia  kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki
 
Habari ni kwa hisani ya  IKULU Blog