Thursday, January 31, 2013
SIRI NZITO: MGOGORO WA GESI
MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa
Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani
humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo,
nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.
Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.
Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:
“Pamoja na hayo nikachukua maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya.”
Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.
Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha uchochezi kwa makundi ya watu.
Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Waziri Mkuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Masoud Mbengula alikiri chama hicho kumeguka na akataja sababu kuwa ni makundi yaliyotokana na uchaguzi wa ndani uliofanyika mwaka jana.
“Tusiwe wanafiki, ni kweli kuna makundi ndani ya chama… wabunge hawako pamoja na ndiyo hali iliyotufikisha hapa… suala hili lipo wazi kabisa,” alisema Alhaji Mbengula.
Kamati ya Spika hatihati
Akizungumzia Kamati ya Bunge iliyotarajiwa kuundwa na Spika kwenda Mtwara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wa huko, Pinda alisema hawezi kuingilia mhimili huo wa Dola isipokuwa atatoa taarifa bungeni na kama Spika ataona wabunge wameelewa, basi ataamua lolote.
“Nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia jambo hili ndani ya Bunge na Spika akiona wabunge wamenielewa bila shaka atasitisha lakini akiona bado inafaa ataamua yeye,” alisema.
Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Mawaziri wanaotoka Mkoa wa Mtwara ambao ni George Mkuchika (Utawala Bora) na Hawa Ghasia (Tamisemi) pamoja na wawekezaji wa kutoka China ambayo alisema yalilenga kuwapa halihalisi ya huko.
Nchimbi afunguka
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema vurugu hizo zimefikia mwisho na Serikali haitavumilia tena machafuko ya aina hiyo.
Dk Nchimbi alisema timu ya wataalamu ipo Mtwara kuweka mambo sawa na kusema Serikali itatimiza majukumu yake pasi na shaka yoyote na kusisitiza kuwa haiwezi kukubali Tanzania ikawa vipande.
Alisema Serikali inafanya tathmini kujua hali ilivyo Mtwara na ikibidi itasitisha shughuli zote za kisiasa mkoani humo.Mtwara wampinga
Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wamegawanyika baada ya ziara ya Waziri Mkuu baada ya baadhi yao kupinga mpango wa Serikali wa kusafirisha gesi asilia kwa bomba kwenda Dar es Salaam.
Katika ziara yake, Waziri Mkuu alitoa ufafanuzi juu ya manufaa yatakayopatikana mkoani Mtwara kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kiasi cha kumshangilia na kumpigia makofi.
Shura ya Maimamu Mtwara imesema jana kwamba haijaridhishwa na majibu iliyoyaita mepesi ya Waziri Mkuu katika hoja nzito na kwamba bado Serikali haijaupatia suluhu mgogoro huo.
“Baada ya kutoka pale tulifanya kikao kupitia maelezo ya Waziri Mkuu, kuna maeneo hatujaridhika … amezungumzia ‘powerplant’ (mtambo wa kufua umeme) kama mtambo wa kusafisha gesi, ndiyo aliousema utajengwa Madimba… lakini sisi tunahitaji ‘powerplant’, mashine za kufua umeme pamoja na hiyo ya kuchakata gesi iwe Mtwara… katika eneo hilo hatujaridhika,” Msemaji wa Shura hiyo, Sheikh Abubakar Mbuki alisema na kuongeza:
“Waziri Mkuu asituambie tu gharama za kutandaza nyaya ni kubwa kuliko bomba la gesi akaishia hapo. Atuambie gharama hizo ni kiasi gani badala ya kusema ni gharama kubwa… mbona gharama za bomba zipo wazi, kwa nini hizi za nyaya hazisemwi?”
Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Katani Katani alisema “Sijaelewa kabisa… nashangaa watu wanashangilia wakati madai yetu ya msingi hayajapata ufumbuzi… dai letu la kwanza lilikuwa viwanda vya kuchakata gesi vijengwe Mtwara, hilo limepatiwa ufumbuzi, la pili lilikuwa mitambo ya kufua umeme Megawati 600 ijengwe Mtwara.”
“Hili hajalipatia ufumbuzi, tunachokataa sisi wana Mtwara ni kusafirisha gesi kwa njia ya bomba, tunataka mashine zinazojengwa Kinyerezi zihamishiwe Mtwara… kutuambia kupeleka umeme Dar es Salaam kwa njia ya nyaya ni gharama kubwa hilo sikubaliani.”
Alisema kutokana na kutopatikana kwa ufumbuzi wa dai hilo moja, bado wananchi wa Mtwara wataendelea kupinga mradi huo.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake juzi, Pinda alisema gesi ghafi haitasafirishwa kwa bomba kwenda Dar es Salaam na badala yake usindikaji utafanyika Mtwara.
“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yeyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu… kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba, gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema Pinda na kuongeza:
“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme… tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”
MWANANCHI
RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KABILA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya Januari 30. 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es
salaam jioni ya Januari 30. 2013
PICHA NA IKULU
Wednesday, January 30, 2013
HAYA NDIO MANENO ALIYOYASEMA MWIGIZAJI LULU NJE YA MAHAKAMA KUU.
January 29 2013 ndio msajili
amethibitisha kwamba mwigizaji Lulu ametimiza masharti yote ya dhamana
juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia.
Lulu na mama yake mzazi wote
kwa pamoja waliangua vilio baada ya dhamana yao kukamilika wakati wakiwa
nje ya Mahakama kabla ya kuondoka na Lulu kuingia uraiani.
Haya ni maneno ya Lulu
aliyoyatoa akiwa analia…. “Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu
waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari
ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na
zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu”
Tuesday, January 29, 2013
KINANA NA UJUMBE WAKE WAKAGUA UJENZI DARAJA LA MALAGARASI KIGOMA
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk, Asha Rose Migiro na Asha Baraka wakiwa mstari wa mbele kwenye matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Wananchi wa Nguruka wakisema wakati msafara wa Kinana wa ujumbe wake ukipita kwa matembezi kuingia katika mji huo mdogo kufanya mkutano wa hadhara Wananchi husuasan kina mama wakishangilia msafara wa Kinana upoingia Nguruka
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa hadhara wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela akihutubia mkutano huo wa Nguruka mkoani Kigoma Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka Mamia ya wananchi wakimsilikiza Kinana kwenye mkutano huo Mkazi wa Nguruka akimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo huku akiwa amepozi kwenye baiskeli yake Kinana akiwaaga wananchi wa Nguruka baada ya mkutano huo. Pamoja naye ni Dk. Asha-Rose Migiro. Baadaye Kinana na ujumbe wake alienda kwenye mkutano mkubwa mwingine uliofanyika mji wa Uvinza. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Subscribe to:
Posts (Atom)