Pages


Photobucket

Saturday, June 1, 2013

DIAMOND AENDELEA KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA KIMAPENZI, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
DIAMOND ANAFAFANUA

“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER

Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA

Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.

“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”Chanzo:www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment