Pages


Photobucket

Wednesday, June 26, 2013

TAKWIMU KOMBE LA MABARA: TORRES BADO BAO 1 KUIFIKIA REKODI YA RONALDINHO - SPAIN NDIO TIMU ILIYOCHEZA MICHEZO MINGI BILA KUFUNGWA - LUIS SUAREZ AMUONDOA KWENYE KILELE CHA MABAO FORLAN

Hatimaye jana usiku timu nne zitakazocheza nusu fainali ya kombe la mabara zimejulikana kwa Spain kuikanya 3-0 Nigeria huku Uruguay nao wakijipigia 8-0 Tahiti. Hizi zifuatazo ndio takwimu zilizotengenezwa kupitia michezo hiyo.

- Spain jana usiku wameweka rekodi ya kutokufungwa kwenye 28 za mashindano, hii ni rekodi mpya wakiivunja ile ya mechi 27 iliyowekwa na Ufaransa.

- Timu zote zilizoingia kwenye nusu fainali ya kombe la mabara - tayari wameshawahi kubeba ubingwa wa kombe la dunia. 

- Spain wameweza kufunga katika mechi ya 15 mfululizo. 

- Mabao manne ya mshambuliaji wa Uruguay - Hernandez, yamemfanya awe mchezaji wa nne kufunga mabao manne katika historia ya kombe la mabara. 

- Fernando Torres sasa amefunga jumla ya mabao 8 katika historia ya kombe la mabara, amebakiza bao moja kufikia rekodi ya wafungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo Ronaldinho na Cuauhtemoc Blanco wenye mabao 9 kila mmoja.

- Ushindi wa Uruguay wa 8-0 dhidi ya Tahiti, umeifikia rekodi yao ya ushindi mkubwa kabisa katika michuano ya FIFA (1950 FIFA World Cup v Bolivia)

- Luis Suarez sasa ametimiza mabao 36 akiwa na jezi ya Uruguay, hivyo kujiwekea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Uruguay - akimfunika Diego Forlan mwenye mabao 35.

chanzo-shafiidauda.com

No comments:

Post a Comment