Pages


Photobucket

Thursday, June 20, 2013

CHECK HAPA LADY JAY DEE ALIVYOOGESHWA PESA NA MASHABIKI WAKE: BOX KUBWA LA KILIMANJARO LAJAA:



Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 11:00 ASUBUHI ONYESHO la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13 katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo
 katika eneo la maegesho ya magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu. Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake.

Jide akikumbatiana na Profesa Jay


Jay akipagawisha


Jay akisema na nyomi ANGALIA PICHA NYINGINE HAPO CHINI     


Mzee Kitime akimpiga picha Komando Kalala wakati anaimba 


Komando Kalala na mkewe jukwaani


Msanii Mango Star na nyoka


Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo. Kufika saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi. Saa 5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado, Yeye,

Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy katika awamu ya kwanza. Baada ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani. Jide alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu, lakini alisisimua mashabiki ile mbaya. Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide. Kutoka hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na kuurusha umati ile mbaya.



KR Mulla


Sir Nature


Nature na Doro
Sinta akimpiga picha Nature
Wakati Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie.    Nature kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake Ngwair apumzishwe kwa amani peponi. Ndipo Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala, Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage. 







TK wa M Band...


Maeneo kama haya Mh Sugu huwa si mkali...anajua kutabasamu


Rapa kutoka Ukonga


Alikuwepo...Mgaya Kingoba Mhariri wa Michezo gazeti la Habari Leo


Kutoka kulia Baraka Msilwa, Francis Kifukwe na mkewe

Wanaume walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia. Ikawadia zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee, baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi, Nikusaidiaje na Kamili Gado. Watu kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa kukanyaga’. Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa.

No comments:

Post a Comment