Pages


Photobucket

Monday, June 24, 2013

Mtoto: Nilipigwa risasi na polisi


ARUSHA-TANZANIA,
Wakati watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa, amedai kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo. 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kampeni wa chama hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani yaliyodhuru ubongo wake.
Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo.
Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma. Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.

No comments:

Post a Comment