Pages


Photobucket

Thursday, June 20, 2013

Msimu Wa Shindano La Epiq Bongo Star Search Wazinduliwa Jijini Dar Leo.

Mkurugenzi wa Benchmak Productions na Jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi juu ya uzinduzi wa msimu mpya wa EBSS. Kushoto kwake ni Afsa Biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Meneja wa Kampeni wa Push Mobile, Rodney Rugambo akielezea namna usaili kwa njia ya simu utakavyofanyika
Mshindi wa Epiq BSS 2012, Walter Chillambo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu mpya wa EBSS. Anayemfuatia kulia ni Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, na Ritha Paulsen, Mkurugenzi wa Benchmark Prouductions
Mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo akipeana mkono na Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa EBSS. Anayetazama ni kulia, ni jaji mkuu wa EBSS, Ritha Paulsen
====== ======= ========
ZANTEL YAZINDUA MSIMU WA SABA WA EPIQ BONGO STAR
SEARCH
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo
imezindua msimu mpya wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, mwaka huu
ikiwa imejipanga kuwapa vijana wengi zaidi fursa ya kuonyesha na kuendeleza
vipaji vyao.
Msimu huu mpya,ambao utakuwa msimu wa saba toka
shindano hilo lianzishwe mwaka 2006, unatarajiwa kujumuisha wadau wakubwa wa
muziki, hivyo kusaidia kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi pamoja na
kuwajengea ushirikiano utakaowasidia kuendeleza kazi zao za muziki baada ya
mashindano.
Shindano la mwaka huu litakuwa na kauli mbiu ya
‘KAMUA’ ikimaanisha kutumia uwezo wako wote katika kufanya kile unachopenda, litaenda
kufanya usaili kwenye mikoa sita ya Mbeya, Arusha, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na
Dar es Salaam.
Kwa mwaka jana shindano la Epiq BSS lilipata
mafanikio makubwa hasa kwa idadi kubwa ya vijana kujitokeza kufanya usaili, na
kubwa zaidi ikiwa ni vijana wote walioingia kumi na mbili bora kufanikiwa kutoa
nyimbo zao ambazo zimefanya vizuri.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen amesema mwaka huu
wana mpango wa kuwafikia vijana wengi zaidi lakini pia kutengeneza wasanii
nyota wengi zaidi ukiacha mshindi.
“Sote ni mashahidi wa namna shindano hili lilivyopata mafanikio toka
ilipozinduliwa miaka saba iliyopita, na hakika kila mwaka tumekuwa tukisogea
mbele zaidi, na mwaka huu mpango wetu ni kuzalisha wanamuziki watakaofanikiwa
wengi zaidi’.
Shindano la mwaka huu pia litakuwa na vitu
vingi vipya, ikiwemo ongezeko la jaji mmoja katika usaili wa mikoani, ambapo
jaji huyo atakuwa ni mdau wa mziki kutoka mkoa husika.
‘Kwenye kila mkoa tutakakoenda kufanya usaili tutakuwa na jaji mwenyeji
ambaye tunaamini atasaidia kuongeza ladha ya machaguo ya vipaji na hivyo
kuhakikisha tunapata vipaji aina tofaouti’ alisema Paulsen.
Naye Afsa biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan
amesema uzinduzi huu wa leo ni furaha kubwa kwa kampuni ya Zantel kwani
unaashiria ufunguzi wa milango ya kuwasaidia vijana wengi wa kitanzania
kutimiza ndoto zao.
‘Kwa mwaka jana pekee Epiq BSS ilifanikiwa
kusaili vijana zaidi ya elfu hamsini, jambo ambalo linaonyesha kitu kimoja,
kuna uhitaji wa kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza vijana’ alisema Khan.
Ikitekeleza ahadi yake ya
kuwasaidia vijana baada ya shindano, kampuni ya Zantel iliwarekodia wimbo mmoja
mmoja washiriki wote waliongia kumi na mbili bora, ikiwa ni pamoja na kuwapa
ziara ya kujitangaza kwenye mikoa mitatu.
‘Tumefanikiwa kuwajengea vijana
hawa msingi wa kazi yao ya muziki, na tuna furaha kusema wengi wao hadi sasa
wanafanya vizuri, na huu ndio aina ya udhamini kampuni ya Zantel inapenda
kujihusisha nao’ alisisitiza Khan. Mshindi wa mwaka huu pia atajinyakulia milioni
hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Katika kuwapa fursa vijana ambao hawatafikiwa
na majaji, Zantel pia itafungua laini za kurekodi kwa simu toka siku ya kwanza
ya kuanza usaili mikoani, ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 ili
kujirekodi kwa njia ya simu, au kutuma neno KAMUA kwenda 15530 kupata maelezo
zaidi.
Usaili utaanzia Dodoma tarehe 29 and 30 ya
mwezi huu katika ukumbi wa Maisha Club, ikifuatiwa na Zanzibar tarehe 5 na 6
mwezi wa saba katika hoteli ya Bwawani. Mbeya usaili utakuwa tarehe 10 hadi 11
mwezi wa saba pale club Vybes, Mwanza tarehe 14 hadi15 mwezi
wa saba Club Fussion, na Arusha itakuwa tarehe 20 hadi 21 mwezi wa
saba Club Tripple A ikimalizikia na Dar es Salaam tarehe 26 hadi 28 pale Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment