Pages


Photobucket

Tuesday, February 26, 2013

SERIKALI YAISHUKIA TFF, YAZUIA KATIBA MPYA KUTUMIKA

 
Serikali Yaishukia TFF, Yazuia Katiba Mpya Kutumika

Na Thehabari.com

SERIKALI imeingilia suala la uchaguzi wa Shirikisho la  Michezo nchini Tanzania (TFF) na kuamua kuifuta katiba  ya shirikisho hilo inayotumiza hivi sasa ambayo  ilirekebishwa mwaka jana (2012) pamoja na kuagiza ifuatwe katiba ya awali ya mwaka 2006. Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara  akuzungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuitaka TFF iitishe Mkutano Mkuu kama inataka kufanya marekebisho ya Katiba yake. Katika ufafanuzi wake Dk. Mukangara ameagiza TFF kufuata sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania  (BMT) ikiwa inataka kufanya marekebisho ya katiba yake.

"Naelekeza na ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha  michezo nchini kilicho juu ya BMT. TFF wafanye uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya  mwaka 2006 kwa kuzingatia sheria na kanuni za baraza la michezo la Taifa," alisema Dk. Mukangara.

Akifafanua zaidi Dk. Mukangara alisema baada ya wataala kupewa kazi yakuangalia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya TFF na mgogoro wa uchaguzi unaoendelea, wizara imebaini; sheria Na. 12 ya BMT na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971, pamoja na kanuni za BMT za usajili Na. 442 za mwaka 1999 zimekiukwa.

"...Ha kanuni ya BMT Na. 11(1) inayoeleza wazi utaratibu wa marekebisho ya katiba; 'haukufuatwa'. Kimsingi TFF walitakiwa wajaze fomu Na. 6, 7, 8 na 9 kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT. Sasa TFF hawakufuata taratibu nilizozielekeza kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT," alisema Waziri huyo mwenye dhamana ya Michezo Tanzania.

Aidha Serikali imeitaka TFF na Msajili wa Michezo Tanzania kuwajulisha FIFA ambao walikuwa wameingilia mgogoro huo uamuzi uliofikiwa na Serikali ili nao wajue kinachoendelea kwa sasa.

Saturday, February 23, 2013

MWILI WA MTU ALIYEFARIKI WAKUTWA JALALANI TEGETA -KONDO ,DAR ES SALAAM

Picture
 
 
Aliyetoa picha za tukio hili, Lukansola via JamiiForums.com amefahamisha maelezo yafautayo:
Mwili wa mtu huyu ulikutwa umetupwa maeneo ya Tegeta-Kondo ndani ya uzio wa kiwanja karibu na makaburi ya Kondo juzi tarehe 21-02-2013 sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa kama anavyoonekana.

Polisi walikuwepo wakiwahoji wakazi wa nyumba iliyo ndani ya uzio huo.

Nimeongea sasa hivi na mtu wa maeneo hayo kujua kilichojiri, ni kwamba huyo mtu alikuja kutambuliwa, ni mzee aliyekuwa mlinzi kwenye baa ya mzee mmoja anaitwa Mwaipopo iko maeneo ya Bahari Beach, baada ya kutoonekana kazini watoto wa huyo mzee katika kufuatilia ndo wakaja kugundua ndiye aliyekuwa amekufa pale (walimtambua baada ya kufukuliwa) ingawa ilibidi azikwe maeneo hayohayo kutokana na mwili wake kuwa umeharibika sana.

Huyo mzee alikuwa anaitwa mzee Denis na hakuwa na mtoto wala mke, na kwa taarifa nilizopewa ni kuwa alikuwa mlevi wa pombe za kienyeji, mlevi sana kiasi kwamba chakula kwake ilikuwa sio muhimu.

Taarifa nyingine ni kuwa mama aliyekuwa anaishi kwenye nyumba hiyo alikuwa anauza pombe za kienyeji. Mama huyo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano lakini taarifa inasema kuwa aliachiwa baadaye.

NECTA yatolea ufafanuzi tuhuma na madai ya Shule ya Green Acres

Picture



MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARY 23, 2013

 
 
 



Wednesday, February 20, 2013

KIFO CHA MKONGWE WA MOVIE (MZEE : JUSTUS ESIRI) WA NCHINI NIGERIA CHALETA HUZUNI KUBWA....


justus-esiri Dr-SID-DAD
                                         
Nollywood movie industry has been hit with another sudden death and it’s veteran actor Justus Esiri.
He passed way on Monday night after a short-time battle with an undisclosed ailment in his hometown.
Few months ago, Nigerian singer and Mavin record member, Dr Sid introduced Justus Esiri as his father. Dr Sid real name is Onoriode Esiri, he is the youngest child of the deceased.
As at the time of this report, no detail has been released regarding Justus Esiri’s death but it is a shock to everybody as the family only released this few hours ago.
A source said the now late Justus Esiri has been secretly battling an age related illness for a while but his family chose to make it a secret until his sudden demise Monday night at the age of 71.
Last year over four top Nollywood stars including Pete Eneh and Enebeli Elebuwa died.
Pete Eneh died of untreated leg infection on November 15, 2012 at a private hospital in Enugu while Enebeli Elebuwa died of stroke on the 4th of December 2012 at a private hospital in New Delhi, India.
Just this last week two Nollywood actors died tragically. A source who claimed the angel of death has visited Nollywood might be proven true with the sudden demise of top Nigerian movie stars one after the other within the past 12 months.
Before his death, Justus Esiri was a member of the Order of Niger (MON). He came into limelight in the early 80′s through the popular Village Headmaster TV series. He has also featured in many interesting Nollywood movies.
The late Justus Esiri was born in November 1942 in Oria, Abraka, Delta State. His studied at Catholic Secondary school in Warri in year 1948 before proceeding to Maximillan University in Munich, German in 1964.
He also attended Prof. Weners Institute of Engineering, West Berlin, 1967 and the Ahrens School of Performing Arts in 1968.
Justus Esiri, detoured into motion picture production in 1968 as a staff of the Schiller Theater, Berlin, Germany, where he stayed till 1976. During the 1977 FESTAC held in Lagos, he choreographed the Modern Dress exhibition.
He was Production Manager for Dinner With The Devil. He worked as News translator and Newscaster with the Voice of Nigeria (German Service).

MKUTANO WA CHADEMA WA UZINDUZI WA KANDA YA ZIWA

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kanda ya Ziwa.


Kamanda Alphonse Mawazo akiongea katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kanda ya Ziwa.






HII NI HATARI...................



KAMALA AWA MWENYEKITI WA MABALOZI WA AFRIKA

Balozi Joel M Nheleko wa Swaziland nchini Ubeligiji, ambaye alikuwa Rais wa Mabalozi wa Afrika nchini Ubeligiji aliyemaliza muda wake, akimkabidhi Balozi wa Tanzania Dk. Diodorus Kamala mfuko wenye vitendea kazi kama ishara ya kumkabidhi Urais wa Mabalozi wa Afrika Ubeligiji jijini Brussels.


Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk. Diodorus Kamala ameteuliwa na mabalozi wa nchi za Africa wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo kuwa Mwenyekiti wao.
Balozi Kamala amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini Ubeligiji, Joel Nheleko aliyemaliza muda wake. Tanzania itashikilia kiti hicho kwa muda wa miezi sita hadi Julai 1, 2013.
“Nimefurahi kupewa heshima hii, na naamini nitaitumia fursa hii kufahamiana vizuri na mabalozi wenzangu na kuvutia fursa za kiuchumi kwa nchi yetu,” alisema Balozi Kamala.
Wakati huo huo, juzi mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa Tanganyika, walimchagua Balozi Kamala kuwa mwenyekiti wao.
Nchi wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia.
Nchi hizi zimeunganisha nguvu kutafuta wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya Bonde la Ziwa Tanganyika, ambapo eneo la bonde hili lenye wakazi wastani wa milioni 40 wanalenga kuliendeleza kwa ajili ya kujenga miundombinu, kurahisisha usafiri na usafirishaji, kujenga reli mpya na kuendeleza utalii.
Chini ya mpango huu wanalenga pia kuboresha viwanja vya ndege vya nchi wanachama vya Mbala, Kalemie, Bujumbura, Kigoma na Kasanga kwa nia ya kurahisisha usafiri wa anga katika ukanda huu.
Dk. Kamala amekabidhiwa jukumu la kuratibu mpango huu na kwa pamoja watatafuta fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya mradi huu.

RAIS DK.SHEIN ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA PADR EVARISTUS MUSHI

Maziko ya Padre Evaristus Mushi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein leo ameungana na viongozi wa dini, waumini pamoja na wananchi wenye mapenzi mema, katika kutoa salamu ya mwisho kwa mwili wa Marehemu Padre Evaristus Mushi, kwenye Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita.

Mwili wa marehemu Padre Mushi unapumzikwa leo Kitope Wilaya ya Kaskazini B, Unguja .

Friday, February 15, 2013

AISHA MASHAUZI AKABIDHIWA KITAMBULISHO CHA TAIFA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha na msanii wa muziki wa Taarab, Aisha Mashauzi, baada ya kumkabidhi kitambulisho cha Taifa, wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vitambulisho vya Taifa jana mjini Zanzibar. Mashauzi ni miongoni mwa wananchi kutoka Tanzania Bara waliopewa vitambulisho vyao katika hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,kwa mara ya kwanza kwa Upande wa Zanzibar,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje ya Mji wa Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais Kikwete asaini kitabu cha Maombolezo, Atoa heshima za Mwisho Kwa Marehemu Askofu Thomas Laizer



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha leo, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu

MAGAZETI YA LEO TAREHE 15/02/2013


.