MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameamua kuwatosa vinara
wanaotajwa kutaka kuwania urais kupitia chama hicho kutoingia kwenye
Kamati Kuu (CC).
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
Dalili za kuwatosa vinara wanaotajwa kuwania urais 2015, ni kutokana na
hatua yake ya juzi kuamua kutowapendekeza kuwa miongoni mwa majina
ambayo yangepigiwa kura ili kuweza kuingia katika CC.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa ndani na nje ya CCM wanaona hatua ya
Kikwete kutopendekeza majina ya wanasiasa vigogo wanaotaka urais 2015
kupitia chama hicho katika orodha ya watu 42 ili kuwania nafasi 14 za CC
kama mkakati maalumu wa kuwaweka kando.
Hata hivyo, mkakati huu wa Kikwete ulikuwa hatua muhimu kwake kama
kiongozi wa chama baada ya kukwama kuzuia makundi kung’ara katika
chaguzi zilizopita ambapo wafuasi wa Edward Lowassa waliibuka kidedea
kuanzia katika NEC, mikoani na Jumuiya za chama hicho.
Ndiyo maana baada ya kumalizika Uchaguzi wa wajumbe wa NEC, Kikwete
alisita kuunda CC kwa maelezo kwamba waliochaguliwa walikuwa wageni na
alikuwa hawafamu vizuri. Hatua hii ya Kikwete ilitafsiriwa kama mkakati
wa kuzima nguvu ya mojawapo ya kambi.
Hata hivyo, kuna mtazamo tofauti kwamba hatua ya Kikwete kutopendekeza
majina makubwa na yenye nguvu ndani ya CCM kuwania ujumbe wa Kamati Kuu
inaweza ikawa ni njia ya kuwafanya wajumbe wa CC kuwa na kazi moja tu
ambayo ni kuchuja majina ya wagombea badala ya wao pia kuwa washiriki.
Kutoswa kwa vigogo
Katika hali iliyozua gumzo, majina ya wanasiasa vigogo Edward Lowassa,
Benard Membe na Samuel Sitta ha yakuwamo katika orodha ya Rais Kikwete
aliyowasilisha mbele ya NEC ili kupata wajumbe wa CC, ambacho ni chombo
muhimu cha uamuzi ndani ya chama hicho.
Lowassa, Membe na Sitta ndiyo wanaelezewa kuwa na makundi makubwa yana
yowaunga mkono kiasi cha kutishia uhai wa chama hicho katika chaguzi
zijazo.
Makundi ya watu hao yamekuwa hasimu kiasi cha wakati fulani, Kikwete
kulazimika kuunda kamati ya watu watatu chini ya Rais Mstaafu, Ali
Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Pius Msekwa
na Abdulrahman Kinana, ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho kwa sasa ili
kusuluhisha mgogoro huo.
Hata hivyo, kansa ya mgogoro imeendelea na kujipambanua waziwazi na hasa
wakati wa Uchaguzi Mkuu wa chama hicho mwaka jana wakati makundi hayo
yalipopambana kujaza wafuasi wao kwenye NEC kwa lengo la kujipanga kwa
ajili ya uchagzui wa 2015.
Wafuatiliaji wa siasa za CCM wanaamini kukosekana kwa Lowassa, Membe na
Sitta bila shaka ni pigo kwa mbio za wanasiasa hao kutaka kuingia Ikulu
mwaka 2015.
Kwani kama watapenya kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais kupitia CCM
mwaka 2015 watakuwa wamefuata nyayo za Benjamin Mkapa ambaye aliteuliwa
kugombea urais akiwa si mjumbe wa CC.
Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Kikwete walikuwa wajumbe wa CC kabla ya uteuzi wao kugombea urais.
Maoni ya watu mbalimbali
Baada ya CCM kuhitimisha safu yake ya uongozi kwa Halmashauri Kuu ya
chama hicho (NEC) kuchagua wajumbe CC huku kikiwatosa wanaotajwa kutaka
kuwania urais 2015, baadhi ya wasomi wamesema kitendo hicho kinaonyesha
kuwa chama hicho tawala kimedhamiria kujiimarisha.
Wakitoa maoni kwa nyakati tofauti wasomi hao walisema hali ingekuwa
mbaya ndani ya chama hicho kama baadhi ya watu hao wangechaguliwa kuwa
wajumbe wa CC.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala alisema
kutopendekezwa kwa Lowassa, Membe na Sitta kulitarajiwa kwa kuwa
viongozi wengi wa chama hicho walikuwa hawapendi jinsi baadhi ya
wanachama wa CCM wanavyoonyesha wazi dhamira yao ya kuutaka urais.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment