Machafuko makubwa yametokea jana katika kijiji cha Buseresere Wilayani
Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10
kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste
Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na
watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake
kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo
hilo.
Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya
asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa
kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama
wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili
huduma hiyo.
Imeelezwa kuwa Wakristu hao
walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani
kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele
Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.
Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya
nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo
linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la
kuifunga.
Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye
bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA,
ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo
la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia
nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.
Kutokana
na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam
kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya
wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao
walitumia mapanga na majambia.
Hata hivyo wakati mapambano hayo
yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la
tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa
mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati
akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.
Mbali
na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na
Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent
Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika
hospital ya wilaya ya Geita.
Hata hivyo watu wengine watano ambao
majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa
kutokana na hali zao kuwa nzuri.
Jeshi la polisi Wilayani Chato
na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta
uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la
Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa
biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto
uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.
Mkuu wa Wilaya
ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya
polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho
aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi
za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.
Akizungumza
kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said
Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa
na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya
kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya
kidini.
Habari na picha kwa hisani ya Gsengo Blog
No comments:
Post a Comment