Pages


Photobucket

Saturday, February 23, 2013

MWILI WA MTU ALIYEFARIKI WAKUTWA JALALANI TEGETA -KONDO ,DAR ES SALAAM

Picture
 
 
Aliyetoa picha za tukio hili, Lukansola via JamiiForums.com amefahamisha maelezo yafautayo:
Mwili wa mtu huyu ulikutwa umetupwa maeneo ya Tegeta-Kondo ndani ya uzio wa kiwanja karibu na makaburi ya Kondo juzi tarehe 21-02-2013 sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa kama anavyoonekana.

Polisi walikuwepo wakiwahoji wakazi wa nyumba iliyo ndani ya uzio huo.

Nimeongea sasa hivi na mtu wa maeneo hayo kujua kilichojiri, ni kwamba huyo mtu alikuja kutambuliwa, ni mzee aliyekuwa mlinzi kwenye baa ya mzee mmoja anaitwa Mwaipopo iko maeneo ya Bahari Beach, baada ya kutoonekana kazini watoto wa huyo mzee katika kufuatilia ndo wakaja kugundua ndiye aliyekuwa amekufa pale (walimtambua baada ya kufukuliwa) ingawa ilibidi azikwe maeneo hayohayo kutokana na mwili wake kuwa umeharibika sana.

Huyo mzee alikuwa anaitwa mzee Denis na hakuwa na mtoto wala mke, na kwa taarifa nilizopewa ni kuwa alikuwa mlevi wa pombe za kienyeji, mlevi sana kiasi kwamba chakula kwake ilikuwa sio muhimu.

Taarifa nyingine ni kuwa mama aliyekuwa anaishi kwenye nyumba hiyo alikuwa anauza pombe za kienyeji. Mama huyo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano lakini taarifa inasema kuwa aliachiwa baadaye.

No comments:

Post a Comment