Mkurungenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na Rais wa Ufaransa François Hollande wakipatiwa maelezo katika moja ya maeneo waliyotembelea |
"Tunataka hatua za haraka za kulinda na kujenga upya maeneo ya kipekee ya urithi wa kiutamaduni nchini Mali".
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Matiaifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, aliyoitoa Jumamosi
baada ya kuwasili nchini Mali, ikiwa ni sehemu ya harakati za shirika
hilo za kusaidia ulinzi na kukarabati maeneo hayo yaliyoharibiwa
kutokana na mapigano yaliyoanzia maeneo ya kaskazini.
Bi. Bokova ambaye anatembelea Mali akiwa ameambatana na Rais François
Hollande wa Ufaransa, amekaririwa akisema kuwa uhifadhi na ukarabati wa
maeneo hayo ya urithi wa kiutamaduni pamoja na nyaraka mbali mbali za
kiasili ni hatua muhimu kwa umoja wa kitaifa na maridhiano wakati huu
ambapo wananchi wa Mali wanaimarisha misingi ya amani ya nchi yao.
Mkuu huyo wa UNESCO anatarajiwa kuainisha mpango wa utekelezaji wa
harakati hizo za ukarabati wa maeneo ya urithi wa kiutamaduni kwa
kushirikiana na serikali ya Mali ambapo UNESCO itasaidia ukarabati na
uhifadhi.
Atakuwa na mazungumzo na viongozi wa mamlaka mbali mbali kwenye mji mkuu
wa Mali, Bamako na mji wa Timbuktu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mpango huo.
Chazo: unmultimedia.org
No comments:
Post a Comment