Saturday, June 1, 2013
ZAIDI YA WATU 56 WAFARIKI KWA KIMBUNGA TONARDO
OKLAHOMA -MAREKANI,
Kimbunga kikubwa cha Tornado kimeukumba mji wa Oklahoma mapema leo Jumatatu na kubomoa vitalu vya nyumba, shule mbili na kuua takribani watu 91 ikiwa ni pamoja na watoto 20, viongozi wa mitaa wamearifu.
Ofisi ya mtabibu wa serikali imetoa taarifa ya karibuni kuhusu idadi ya waliopoteza maisha lakini idadi hiyo inaongezeka kwa kasi, wakati kikosi cha huduma ya dharura wamesafisha mabaki yote ya nyumba zilizobomolewa pamoja na shule katika kitongoji cha Moore mjini Oklahoma.
Watabiri wa hali ya hewa wamearifu kuhusu uwepo wa upepo mkali wa maili mbili, na helikopta ya habari za televisheni imenasa faneli zito likipita katika vitongoji kadhaa.
Gavana wa Oklahoma Mary Fallin ameviambia vyombo vya habari kuwa kimbunga hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo akiongeza kuwa majeruhi ni wengi na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu umefanyika.
Naye mkuu wa polisi katika kitongoji cha Moore Jerry Sillings amewataka wakazi wa kuondoka katika eneo hilo wakati masuala kadhaa ya kiusalama yakifanyika.(RFI SWAHILI).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment