Kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa Photo AFP / Isaac Kasamani
Kundi
la waasi la M23 la nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
linarejea katika mazungumzo ya amani na serikali ya Kinshasa mwishoni
mwa juma hili mazungumzo ambayo serikali ya nchi hiyo inaona kuwa ni
jambo sahihi katika utatuzi wa mgogoro huo.
M23
chini ya kiongozi wake Bertrand Bisimwa walitangaza uamuzi huo kwa kile
walichosema ni kutokana na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki Moon na Mjumbe wake katika mataifa ya ukanda wa maziwa makuu kuwa
suluhu ya mgogoro huo itapatikana kwa njia ya mazungumzo.
Taarifa ya M23 iliyotolewa juma hili ilibainisha kuwa Rene Abandi ndiye atakayeongoza ujumbe huo wa M23 kuelekea Kampala.
Mashirika
ya kiraia Mashariki mwa nchi hiyo yanaendelea kuhofia jitihada za waasi
hao ambao wanasemekana kuwa wamekuwa wakipanga kuuchukua mji wa Goma
uliopo Mashariki mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment