Asilimia
kubwa
ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na
chunusi
kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi,
na hii husababishwa sana na
mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye
mafuta na
baadhi ya watu wamepata matatizo haya
baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Tatizo
hili limekuwa kubwa kwa baadhi ya watu na kuna wakati mtu ana kosa hata
raha na
kuwa huru kufanya mazungumzo ya ana kwa
ana na mtu kwa kuogopa muonekano wa madoadoa ya ngozi ya uso wake. Leo
tutaenda kuangalia moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya
chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia
gharama
kubwa.
Mahitaji
Unga
wa Riwa
Maji
ya Rose (Rose water)
Maji
safi ya kawaida
Limao
Mafuta
ya Olive (Olive oil)
Hatua ya Kwanza
Chukua
unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye
pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.
Hatua ya Pili
Upake
mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa
na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu
ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya
mafuta na kuacha ngozi kavu.
Hatua ya
Tatu
Nawa vizuri na maji
ya uvuguvugu.
Hatua ya Nne
Paka
Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu.
Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha
madoadoa na kuondoa makovu kwenye ngozi .
Hatua ya Tano
Paka
mafuta ya Olive kwenye makovu, hii
husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.
Mambo ya kuzingatia
Wakati
unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali
ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu
kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki
ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.
hayo maji ya rose yanauzwa madukan au yanapatikanaje?
ReplyDeleteUnga wa riwa ni nini?
ReplyDeletehatujui
DeleteMaji ya rozi yanapatika vp jaman
ReplyDeleteUpuuz havitoi matokeo!!!
ReplyDelete