Pages


Photobucket

Monday, June 24, 2013

Serikali ya Uingereza kuomba radhi na kutangaza kiwango cha fidia kwa waathiriwa wa Vita vya Mau Mau nchini Kenya

Wapiganaji wa Kenya walioshiriki kwenye vita vya Mau Mau dhidi ya Serikali ya Uingereza
Wapiganaji wa Kenya walioshiriki kwenye vita vya Mau Mau dhidi ya Serikali ya Uingereza

LONDON-UINGEREZA,Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuomba radhi pamoja na kutangaza kiwango cha fidia watakayoitoa kwa watu zaidi ya elfu tano raia wa Kenya walioathiriwa na kuteswa kipindi cha vita vya Mau Mau iliyona lengo la kujipatia uhuru wao. 
Hatua ya Serikali ya London kuomba radhi na hatimaye kutangaza kiwango cha fidia inakuja baada ya waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kufungua kesi wakilalamikia utesajwi waliokumbana nao wakati wa vita hivyo. 

Waathiriwa hao wa vita vya Mau Mau kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanapata fidia hiyo baada ya kutokea vita vya kudai uhuru vilivyofanyika katika miaka ya 1950.

Keshi hiyo ya kudai fidia ilifunguliwa na Paulo Muoka Nzili, Wambungu Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara ambapo walitaka kulipwa fidia naa baada ya mahakama kusikiliza shauri lao wakafanikiwa kushinda kesi hiyo na serikali ikatakiwa kuwalipa fidia.

Askari wa Uingereza wanatuhumiwa kuwatesa raia wa Kenya wakati wa vita hivyo vya Mau Mau lengo likiwa ni kuwatisha ili wasiendelee na harakati zao za kudai uhuru wao kutoka kwa Wakoloni wa Uingereza.

Miongoni mwa vitendo ambavyo vilifanywa na askari hao wa kiingereza ni pamoja na vitendo vya uhalifu wa kijisia ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake waliokuwa wanaishi kwenye makambi baada ya kukimbia vita hivyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague ndiye anatarajiwa kutangaza fidia hiyo yenye thamani ya paumi milioni kumi na nne ambapo kila muathirika anatarajiwa kujipatia jumla ya pauni elfu mbili na mia tano.

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Kenya ilionesha watu 90,000 waliuawa kwenye vita hivyo vya Mau Mau kwa kuteswa huku wengine 160,000 waliweka kizuizini bila ya makosa yoyote na kukutana na unyanyasi mkubwa na mateso.(RFI).

No comments:

Post a Comment