Cristiano
Ronaldo anakaribia kukubaliana na Real Madrid juu ya mkataba mpya wa
kuendelea kubaki Santiago Bernabeu - kwa klabu hiyo ya jiji la Madrid
kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wote
kwenye ulimwengu wa soka duniani.
Madrid
wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na wawakilishi wa Ronaldo kwa
dili lenye thamani ya €155 million kwa mkataba wa miaka mitano - mkataba
ambalo utamfanya Ronaldo aweke kibindoni €15m kwa mwaka baada ya
kukatwa kodi - dili ambalo linatajwa kuwa la thamani zaidi katika
historia ya soka duniani.
Ronaldo, ambaye amefunga mabao 201
katika 199 ndani ya misimu minne aliyokaa Santiago
Bernabeu, aliwapa tumbo joto viongozi wa Madrid baada ya alhamisi ya
wiki iliyopita kuandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba: "All the news
about my renewal
with Real Madrid are false."
Ronaldo
ambaye miezi kadhaa huko nyuma aliwahi kukaririwa akisema hana furaha
ndani ya Madrid katika kile alichosema kwamba ni sababu zinazomfanya
asiwe na furaha ndani ya klabu hiyo viongozi wa Madrid wanazifahamu-
sababu ambazo inasemekana zimetokana na sapoti ndogo anayopata kutoka
kwa klabu yake hasa katika mbio za kugombea Ballon
d'Or, pia kitu kingine ni ugomvi wake na mchezaji mwenzie Marcelo.
Madrid
walimsajili Ronaldo kutoka
Manchester United kwa rekodi ya uhamisho ya €94 million wakati wa
kiangazi mnamo mwaka 2009, mara tu baada ya kurudi kwenye uongozi kwa
Raisi Florentino Perez. Kwa sasa Ronaldo analipwa kiasi cha €10m baada
ya kodi.
Wakati
Ronaldo aalipowasili Spain, kulikuwa na kitu kinachoitwa 'Beckham Law',
ambayo iliwaruhusu wageni ambao wameishi nchini humo kwa miaka chini ya
10 na ambao wanavuna zaidi ya kiasi cha €120,000 kwa mwaka kulipa kodi
ya chini kiasi cha asilimia 23 na sio ile ya kawaida ya asilimia 45,
bado ilikuwepo. David Beckham alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kupata
faida ya sheria hiyo baada ya kuhamia Madrid akitokea kupata Manchester
United mnamo mwaka 2003.
Japokuwa baadae serikali ya Spain
ikaifuta sheria hiyo na sasa mkataba mpya wa Ronaldo utakuwa unakatwa
kiasi cha 52% kama kodi. Hivyo, Madrid itabidi watoe package ya €31m ili
baada ya makato Ronaldo abaki na kiasi cha €15m ambacho anakitaka.
Madrid,
wanatambua umuhimu wa kuendelea kuwa na Ronaldo. Klabu hiyo hivi
karibuni imemkosa Neymar, wakati wakionekana kukata tamaa ya uwapata
wachezaji wa Dortmund Ilkay Gundogan na Robert Lewandowski. Wachezaji
wengine ambao walikuwa kwenye hesabu zao kama vile Sergio
Aguero na Radamel Falcao, hawatoenda Madrid pia, wakati Gareth
Bale ni gharama zaidi kumpata na hataki kuomba uhamisho kutoka Tottenham
na huku Edinson Cavani anaonekana kuwa hana thamani ya fedha ambayo
Napoli wanaitaka kutokana mauzo ya Cavani. Hivyo kubaki na Ronaldo ni
jambo muhimu.
Raisi wa klabu hiyo alikaririwa hivi karibuni
akisema kwamba atafanya chochote kuhakikisha Mreno huyo anabakia ndani
ya jiji la Madrid hata kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye
ulimwengu wa soka.
Madrid sasa wapo tayari kumpa Ronaldo
anachokitaka na kumfanya apate fedha nyingi kuliko
Lionel Messi, ambaye analipwa kiasi cha €13m kwa mwaka kabla ya bonasi
ndani ya Barcelona,
na Falcao, ambaye anapata kiasi cha €14m kwa mwaka ndani ya Monaco.
Samuel Eto'o analipwa kiasi cha €20m kwa mwaka na Anzhi Makhachkala,
ingawa dili hilo la mcameroon huyo lina muda wa miaka mitatu tu na kwa
ujumla dili la Ronaldo litampita Eto'o.
Tatizo kubwa na kizingiti
kikubwa katika makubaliano ya mkataba mpya wa Ronaldo na Madrid ni
suala la haki za taswira yake. Cristiano kwa sasa anamiliki asilimia 60
wakati klabu inachukua 40 zinazobakia. Ronaldo anahitaji maboresho
makubwa kwenye suala hili - inaaminika anataka haki zake zote za taswira
yake kwa maana ya asilimia 100 - kitu ambacho Madrid hawakubaliani
nacho. Hapo ndipo makubaliano juu ya mkataba mpya yanapochelewa.
No comments:
Post a Comment