Mkazi mmoja wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi baada ya kukutwa akimbaka binti wa miaka kumi.
Tukio hilo linaelezwa kutokea jana saa nane mchana, pale ambapo mazazi
wa binti huyo alipomsikia mwanaye akilia kwa uchungu, na aliposogea
kujua kulikoni, alimshuudia kijana huyo akiendelea na ubakaji jambo
lililosababisha apige kelele kuomba msaada wa wananchi.
Kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji katika eneo hilo,
mtuhumiwa huyo alijikuta akipokea hasira za wananchi kwa kupigwa na
kunusurika kuchomwa moto baada ya baadhi ya wananchi wengine kushauri
afikishwe polisi.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Iringa akivuja damu kichwani.
No comments:
Post a Comment