BABA wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la
miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha
kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.
“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walifunga safari mpaka
nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri
kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.
“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali
ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu
lakini hajawahi kuja kuniona.
“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.
No comments:
Post a Comment